Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Manara atoa ahadi ya kulitikisa Bunge

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Simba SC, Haji Manara amefunguka na kutoa ahadi ya kuwa katika msimu ujao wa ligi 2018/19 timu yake itafanya makubwa mpaka kupelekea Bunge kutengua baadhi ya kanuni zake

Manara ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii mara baada ya uongozi wa Simba kiujumla kuhudhuria shughuli za Bunge kwa siku ya leo kutokana na mualiko waliopewa na Spika wa Bunge Job Ndugai katika siku za hivi karibuni.
"Mabingwa wa nchi ndani ya mjengo, asanteni Wabunge wote kwa heshima kubwa mliyotupa leo. Nawaahidi mwakani kwa tutakayoyafanya mtatengua kanuni ili tuingie ndani na kuwa sehemu ya Bunge", amesema Manara.
Simba sasa imefikisha alama 68 kileleni katika michezo 28 ikiwa imebakiza mechi mbili kuweza kumaliza msimu huu.


Kikwete aishauri Yanga SC

Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kuweka wazi kuwa klabu Yanga inahitaji mfumo sahihi wa uendeshaji wa mpira ambao utaweza kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za kukosekana kwa pesa ili waweze kufanya vizuri katika michezo yao inayowakabiri

Mhe. Ridhiwani ametoa kauli hiyo kupitia moja ya mijadala ambayo ilikuwa inaendeshwa katika mtandao wa kijamii twitter ukiwa na lengo la kutoa hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa wanajangwani kujitokeza kwa wingi viwanjani ili waweze kujikusanyia mapato mengi yatakayotokana na watu kuingia uwanjani na sio kusubiri kuichangia muda ambao itakuwa imekwama kabisa.
"Yanga wanaitaji mfumo sahihi wa uendeshaji wa mpira utaolezea jinsi ya kukabiliana na changamoto ya kukosekana kwa pesa, kuacha kutegemea mtu, kutafuta vyanzo vya mapato vya uhakika, kulipa pesa kwa wakati na mengineyo yanayohusu mfumo wa mafanikio katika soka", ameandika Ridhiwani.
Licha ya Ridhiwani kutoa ushauri kwa Yanga lakini mmoja ya wadau waliokuwa wanachangia mjadala huo amesema "ukianza kuusaka huo mfumo bora wa kuindesha Yanga ndio wanatokea kina Akilimali wanaleta fujo, timu ikipoteza 'direction' nao wanakaaa kimya, 'so long as' kuna watu wana maslahi binafsi ndani ya Yanga, mabadiliko ni ngumu sana kuyapata".
Klabu ya Yanga katika msimu huu wa mwaka 2017/18 imeonekana ikipitia maisha magumu sana katika uendeshaji wa timu hiyo kwa kile kinachodaiwa kukosekana kwa pesa za kulipa mishahara ya wachezaji na makocha jambo ambalo limepelekea Yanga kufanya vibaya katika michezo yake huku wengine wakishindwa kujua ni nini wanapaswa kufanya ndani klabu hiyo ili waweze kuikoa katika shimo waliloingia.


Manara aweka nia kuisaidia Yanga

Afisa Habari wa timu ya Mabingwa Tanzania Bara, Haji Manara ameweka nia yake ya kutaka kuandaliwa mechi kati ya Simba  na watani zao wa jadi Yanga ili waweze kuwasaidia kiuchumi kwa kuwapatia mapato yatakayokusanywa katika mchezo huo

Manara ameyasema hayo ikiwa ni katika kuendeleza utani wake kwa klabu hiyo ambayo imeshindwa kutetea ubingwa wake katika msimu huu huku ikidhaniwa kwamba ni kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayopitia klabu hiyo.
Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram leo ameweka picha ya gari la klabu ya Yanga ambalo likionekana limepata hitilafu  na kusema kwamba kati mechi hiyo sharti wanalotoa kwa watani zao ni kuwapa shikamoo Simba.
"Nina jaribu kuongea na wenzangu klabuni tuone namna ya kucheza mechi ya kirafiki na hawa jamaa ili wachukue mapato yote ya uwanjani kuwanusuru na swaumu yao..hata sijui kama bima imelipiwa hii gari" Manara.
Ameongeza "Sharti la hiyo mechi Gongowazi wote watuamkie..Shikamoo Simba.


Ukiacha Yanga, Hii ni Timu Nyingine kubwa inavyomtaka Adam Salamba

Afisa Habari wa Timu ya Lipuli ya Iringa Clement Sanga leo ametaja kilabu kingine kikubwa cha Tanzania kinachotaka kumsajili mchezaji wao Adam Salamba

Yanga ndio wa kwanza kuandikia barua klabu ya Lipuli kuonesha nia yao ya kumtaka mchezaji huyo, lakini kipo kilabu kingine tena kikubwa ambacho kimemtaka mchezaji huyo kwa barua

Tazama hapo chini, Clement Sanga akiongea


Kikwete anautaka Uenyekiti wa Yanga?

Ikiwa ni siku moja imepita tangu shirikisho la soka nchini (TFF), liitumie barua Yanga ya kuitaka kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi zilizopo ikiwemo ya Mwenyekiti, mapya yameibuka yakimhusisha Ridhiwani Kikwete kuitaka nafasi hiyo

Baada ya tetesi hizo, Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze amesema hana lengo la kutaka uongozi ndani ya klabu hiyo kwa sababu yeye ni shabiki na hana kadi ya uanachama wa Yanga hivyo hana sifa za kugombea uongozi.
“Sina lengo lolote la kutaka uongozi ndani ya Yanga labda wanachama wenyewe ndio wanatengeneza maneno hayo lakini mimi binafsi hakuna sehemu nimewahi kutamka kwasababu hata sifa tu sina mana sina kadi ya uanachama,'' amesema.
Aidha Ridhiwani ameongeza kuwa mara kadhaa watu wa Yanga wamekuwa wakiomba ushauri juu ya nini cha kufanya na amekuwa akishauri kama shabiki wa kawaida na hajawahi kuwaambia kama anahitaji kuwa kiongozi.
Yanga imeitisha mkutano mkuu wa wanachama mwezi ujao na huenda agenda kubwa ikawa ni uchaguzi kuziba nafasi ya Mwenyekiti ambayo ilikuwa inashikiliwa na Yusuf Manji kabla ya kujiuzulu mwaka jana.


TFF wazijibu Hoja za Richard Wambura

Shirikisho la soka nchini TFF limejibu tuhuma zilizotolewa na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michael Richard Wambura, baada ya hukumu ya kufungiwa maisha kutangazwa dhidi yake na kamati ya maadili inayoongozwa na mwenyekiti Hamidu Mbwezeleni.

Wambura alizungumza na waandishi wa habari kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake, huku akiweka wazi  baadhi ya mambo ambayo anaamini yamekua mzizi wa yeye kufanyia figisu hadi kuingizwa hatiani.

Mdau huyo wa soka alidai kuwa, kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya TFF likiwepo suala la ubadhilifu wa fedha, ambao umekua kinyume na utaratibu, jambo ambalo aliahidi kulitafutia siku la kulianika hadharani kupitia vyombo vya habari.

TFF imejibu tuhuma hizo kwa kutoa ufafanuzi wa kina katika kila kipengele ambacho kilizungumzwa na Wambura alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.


1.Matumizi mabaya ya fedha za TFF
JIBU : Wambura kama Mwenyekiti wa kamati ya fedha amehudhuria vikao zaidi ya 4 vya kamati na hajawahi kulalamika kokote mpaka amefungiwa.

Bajeti ya TFF iliyopitishwa Dodoma kwa Mwaka Mzima ni Bilioni 8.6 hivyo matumizi anayosema ya Bilioni 3 kwa miezi 7 yanaonyesha jinsi gani TFF inavyopambana na changamoto za kifedha hivyo kuhakikisha inapunguza matumizi.

Mapato yaliyopatikana kwa miezi Saba (7) iliyopita yalitumika katika maeneo yafuatayo :

Timu ya Taifa Taifa stars(Fifa dates),Kilimanjaro Stars  (Challange Cup),Kambi kwa Timu ya Taifa Under23, Kambi U20, U16, Wanawake U20, Ligi za Wanawake, Kombe la Shirikisho la Azam, kozi za makocha,kozi za waamuzi za nje na ndani, vikao vya kamati ya utendaji na  kamati ndogo ndogo, mishahara ya watumishi wa TFF na makocha wa timu za Taifa, kulipa madeni tuliyoyakuta na kuidhinishwa na kamati ya fedha, kozi za Grassroots na Live Your Goal na soka la Ufukweni

2.Ajira za TFF watu kupewa kwa kujuana.
JIBU : TFF haijawahi kuajiri nafasi yoyote ile zaidi ya Wakurugenzi 3 na meneja 1 tofauti na uongo unaozungumzwa,Wakurugenzi walioajiriwa ni Mkurugenzi wa Fedha,Mkurugenzi wa Mashindano,Mkurugenzi wa sheria na Wanachama na Meneja Masoko,katika kupunguza matumizi ya fedha Taasisi imebaki na Wafanyakazi 21 kutoka 44 wa awali waliokutwa na Ndugu Karia.

3.Kumteua Wilfred Kidao kuwa kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
JIBU : Kaimu Katibu Mkuu alikaimishwa na Kamati ya Utendaji na yeye Wambura akiwa mmoja wa waliompitisha.

4.Mipira 100 kila mkoa kwamba kuna watu wamepiga fedha za TFF.
JIBU : TFF chini ya Rais wa TFF aliyekuwepo madarakani Ndugu Wallace Karia haijawahi kununua mipira,mipira iliyotolewa ilinunuliwa na uongozi uliopita ilichofanya TFF ni kuigawa kama ilivyofanya.

5.Kuwa na wafanyakazi wawili kwenye nafasi moja.
JIBU : TFF haijawahi kuajiri mfanyakazi zaidi ya mmoja kwenye nafasi moja,wengi waliokuwepo kwenye Shirikisho kwa sasa wanajitolea akiwemo Afisa Habari.

6.Suala la Waamuzi kuondolewa kuchezesha ligi kuu.
JIBU : Ili kuongeza ubora wa uchezeshaji TFF ikaamua kuchaguwa waamuzi wa juu(Elite) tofauti na awali ambako kulikuwa na idadi kubwa mchanganyiko ya waamuzi.

7.Kaimu Katibu kutuma majina ya Makamishina.
JIBU : Jina la Michael Wambura na Ahmed Mgoyi ndio yaliyopelekwa kama utaratibu unavyotaka ya kujaza kwenye fomu moja pekee na TFF haikuwahi kubadilisha wala kukata jina la mtu yeyote.

8.TFF ya sasa mpaka uwe na urafiki na watu 3 Karia, Mgoyi, na Nyamlani.
JIBU : TFF haiendeshwi kwa urafiki bali kwa utaratibu wenye kufuata kanuni.

Kikao kilichotoa maamuzi ni Kamati inayojitegemea (Independent) sio rahisi kuingiliwa kwa kuwa hata Rais wa TFF hawezi kuiingilia

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaoenezwa kwa maslahi binafsi,ni vyema watu wakajikita kwenye kujibu tuhuma zao bila kuhusisha uongo na vitu visivyo vya kweli kwa Taasisi ambayo kwasasa ipo makini kwenye kuhakikisha kila kitu kinafuata utaratibu ikiwemo masuala ya kifedha pamoja na mambo mengine.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF.


TANZIA: Kocha wa zamani wa Yanga, Jack Chamangwana afariki dunia

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Jack Chamangwana amefariki dunia hapo jana siku ya Jumapili majira ya jioni kwenye Hospitali ya Queen Elizabeth (QECH) nchini Malawi.

Ripoti zinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni kutokana na shinikizo la Moyo hii ikiwa ni Mwezi mmoja umepita toka kumzika mpwa wake, George Chamangwana.
Wakati wa uhai wake Chamangwana maarufu kwajina la ‘Africa’ alikuwa Mkurugenzi wa ufundi ndani ya klabu ya Be Forward Wanderers ya nchini Malawi.
Nahodha huyo wazamani aliyekuwa na umri wa miaka 61, aliwahi kuifundisha timu ya Yanga mwaka 2006 kabla kutimka zake kwao.
Chamangwana ameanza kuitumikia timu yake ya Taifa ya Malawi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya Julai 10 mwaka 1975 akiwa na umri wa miaka 18 huku goli lake la kwanza akifunga dhidi ya Botswana.


Yanga yaomba radhi

Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligii Kuu Tanzania Bara na wawakilishi pekee nchini Tanzania katika mashindano ya kimataifa Yanga, imefunga na kuiomba radhi kampuni ya SPORTPESA kwa kushindwa kuvaa jezi zao zenye nembo ya mdhamini huyo

Hayo yameelezwa na taarifa zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa jioni ya leo Mei 07, 2018 na kusema sababu kubwa ya wao siku ya jana Mei 06, 2018 kuonekana wakiwa uwanjani na jezi zisizo kuwa na 'logo' ni kutokana na kuzuiliwa na waratibu wa mashindano hayo kwasababu ya kutokuwepo kwa maelekezo ya matumizi ya wadhamini.
"Hivi sasa uongozi wa Yanga na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa pamoja tunashughulikia suala hili ili mechi zijazo nembo ya mdhamini wetu iweze kutumika kama ilivyotumika kwenye michezo ya hatua za awali. Ikumbukwe kwamba kuanzia hatua hii ya makundi, CAF ndiyo inasimamia haki za matangazo pamoja na mabango yote yanayotakiwa kuwekwa viwanjani, hivyo tayari mawasiliano  nao kupitia TFF yamekwishafanyika", amesema Mkwasa.
Pamoja na hayo, Mkwasa ameendelea kwa kusema "uongozi wa Yanga unaomba radhi kwa kampuni ya SPORTPESA na wale wote walioathirika na matatizo yote yaliyojitokeza wakati wa mchezo huo".
Kwa habari kamili soma hapa chini


Ndanda FC wafanyiwa kama Yanga

Klabu ya Simba imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Emmanuel Okwi kulia kwenye picha
Goli pekee na la ushindi la Simba limefungwa na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi kunako dakika ya 43 ya mchezo.
Matokeo mengine ya leo ni klabu ya Arsenal imekubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Stand United,  magoli ya Stand yamefungwa na Sixtus Sabilo na Ally Ally huku la Azam likifungwa na Shaaban Idd.
Kwa matokeo hayo Simba kwa sasa wanakuwa na alama 65 wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 49 na Yanga pointi 48.


Namshukuru Mungu ametujaalia mtoto wa kike, naumizwa na wanaosema nimegoma – Ajib

Straika wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajib amejaaliwa kupata mtoto wa kike huku akisema kuwa anashangazwa na watu wanao mshambulia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwamadai kuwa amegoma kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Algeria kuwakabili USM Alger mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Namshukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwa sababu ujauzito wa Mke wangu ulikuwa na matatizo mengi. Kunawakati nilikuwa na hafu kubwa juu ya maisha yake.
Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu yakufanya hivyo, mpira ni kazi yangu.
Nawasamehe kwasababu wangesikia Mke wangu amefariki kwa matatizo ya uzazi nadhani wangesema mengi.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga kimesafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya USM Alger utakao pigwa hapo kesho siku ya Jumapili huku wachezaji wake nyota, Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshimbi na Kelvin Yondani wakikosekana kwenye kikosi hiko kwa sababu mbalimbali.


Manara: Ajib ni mzuri mara tatu zaidi ya Samatta

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara amesema kwamba mchezaji wa timu ya Yanga Ibrahimu Ajib ni mzuri lakini hapendi kufanya mazoezi na pia kubaki katika kiwango bora kwa muda mrefu

Manara amezungumza hayo  April 18, katika kipindi cha KIKAANGONI  kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za kijamii ya EATV na kuongeza kwamba licha ya kipaji alichonacho lakini anashindwa kukilinda kwa kufanya juhudi mazoezini
“Ibrahim  Ajib anaanza vizuri msimu halafu ikifika mahali akishakua Mfalme katika timu anapumzika, halafu Ajib hapendi mazoezi, hawezi kucheza mechi saba mfululizo katika kiwango cha juu kwasababu hapendi mazoezi , kama angependa mazoezi ni mzuri mara tatu zaidi ya Mbwana Samatta”, alisema Manara
Kwa upande mwingine Manara amesisitiza kwamba Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye nidhamu ukilinganisha na wachezaji wengine waliotoka timu ya Simba na kuhamia kwa wapinzani wao Yanga.


Shabiki wa Simba aliyetoa taulo kwenye goli la njombe mji afariki dunia

BREAKING NEWS
Taarifa isiyo rasmi Shabiki wa timu ya Simba mkoani Njombe alietoa kitaulo cha mlinda mlango wa timu ya Njombe Mji amekutwa amekufa nyumbani kwake mgenderwa leo huku sababu ya kifo hicho bado hakijafahamika.
Baada ya vurugu za kitaulo pale uwanjani Sabasaba juzi alikamatwa na polisi na kuachiwa jana.
Goli kipa wa Simba amepost kuonyesha kafariki, Tazma video hapo chini:_


Mashabiki wa Njombe Mji "wahamia" Simba

Klabu ya Simba imefanikiwa kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya klabu ya Njombe Mji kunako dimba la Saba saba mjini Njombe.


Magoli yote mawili ya Simba SC yamefungwa na John Bocco kunako dakika ya 17 na 64 ya mchezo huo.
Kwa matokeo hayo, Simba kwa sasa inaongoza ligi kwa alama 49 ikifuatiwa na mahasimu wao Klabu ya Yanga yenye alama 46.
Baada ya Mechi Mashabiki wakafunguka wakiwemo wa Njombe mji ambao wanaifagilia Simba, Tazma video hapo Chini:-


Anusurika kuuawa Baada ya Kuchukua Taulo la Golikipa wa Njombe Mji Uwanjani

Shabiki ambaye hakujulikana mara moja ameingia uwanjani kisha kukimbilia golini mwa mlinda mlango wa timu ya Njombe Mji, David Kisu na kuchukua taulo lililokuwa golini hapo kisha kukimbia nalo wakati timu hiyo ikicheza na Simba uwanja wa Sabasaba Njombe hii leo

Shabiki huyo anayedhaniwa kuwa ni wa Simba, amelipora taulo hilo na kuruka uzio wa uwanja huo na kukimbia nalo hali iliyozua taharuki uwanjani hapo

Shabiki huyo amekamatwa nje ya uwanja na kuanza kupokea kipigo kidogo kabla ya kuokolewa na askari polisi waliokuwa uwanjani hapo, huku taulo hilo likichomwa moto jambo ambalo limefanyika haraka kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na polisi

Zaidi Tazama Video hii hapa chini:-


Taarifa kuhusu Rufaa ya Wambura TFF

Ile rufaa inayomhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Richard Wambura, imesikilizwa leo kwa pande zote mbili kukutana katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala.

Kwa mujibu wa Wakili wa Wambura,Emmanuel Muga, amesema pande zote mbili zimemaliza vizuri kikao hicho na mambo yamekwenda sawia, kinachosubiriwa tu sasa ni maamuzi ya Kamati ya Maadili kutoa hukumu.

Muga ambaye anamtetea Wambura, ameeleza TFF wamesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo.

Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa kujihusisha na soka baada ya TFF kumfungia kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.

Kamati ya Maadili itakaa na kuandaa rasmi na majibu ya hukumu juu ya rufaa hiyo iliyosikilizwa leo Jumamosi.


Manara azungumza baada ya Niyonzima, Kamusoko na Tambwe kuonekana Gym pamoja

Hapo jana siku ya Ijumaa kulienea kipande cha video kinachowaonyesha wachezaji wa klabu ya Yanga, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe na Haruna Niyonzima wa Simba SC wakiwa pamoja katika mazoezi ya viungo Gym.

Kufuatia video hiyo msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka na kusema kuwa licha ya wachezaji hawa kucheza timu mbili pinzani za Simba SC na Yanga SC lakini wapo pamoja na hivyo ndivyo soka linavyo hitaji.
Very nice..hawa ni pro hasa..wanacheza timu shindani kwenye Soka nchini..wanatoka mataifa tofauti..lakini wapo Gym pamoja…hii ndio Soka..always nawaambia Simba na Yanga ni washindani wa dak 90 na watani wa jadi tu..chuki za kijinga zinaletwa na washamba walozijua hz timu FB. WhatsApp na Instagram..niwatakie heri magwiji wetu…. @thabani_scara_13@tambwe17 @niyonzimaharuna
Wachezaji, Thaban Kamusoko na Amis Tambwe wa Yanga SC wapo katika mazoezi mepesi kufuatia kutoka katika majeruhi yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu wakati kiungo wa Simba SC, Haruna Niyonzima alikuwa akisumbuliwa na kifundo cha mguu kilicho mpelekea hadi kupelekwa nchini India kwa matibabu na hatimaye kurejea nchini.


Maneno ya Haji Manara baada ya Taifa Stars Kupigwa 4-1

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea goli kipa namba moja wa Simba ambaye sasa amejiunga na Taifa Stars Aisha Manula kutocheza leo katika timu ya Taifa dhidi ya Algeria

Manara amesema kuwa Manula leo hakuweza kushiriki katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Algeria ni kutokana na mchezaji huyo kupata jeraha siku ambayo Simba ilicheza na Al Masry. 
"Golikipa namba moja nchini Aishi Manula kuwakosa Algeria baada ya kupata maumivu kidogo ya Enka..jeraha hilo dogo alilipata siku Simba ilipocheza na Al Masry. Nimethibitishiwa taarifa hizi na Tanzania One mwenyewe....tuendelee kuiombea Stars na kuomba afya njema kwa Aishi Manula" alisema Haji Manara 


"Nahama Chama Cha Mapinduzi" - Haji Manara

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kutoa ahadi kuwa endapo klabu ya Liverpool itaifunga klabu ya Manchester United leo basi yeye atahama CCM na kuhamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) 

Haji Manara ametoa ahadi hiyo leo dakika kadhaa kabla ya klabu hizo kushuka dimbani katika uwanja wa Old Trafford huku klabu yake hiyo pendwa ya Manchester United ikiwa nyumbani. 
"Ikitokea Liverpool kuifunga Manchester nahama CCM najiunga na chama cha Hashim Rungwe ..hawatufungi hata kwa bahati mbaya" alisema Haji Manara 
Haji Manara ni mwanachama mzuri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kushika nyazifa mbalimbali ndani ya chama hicho kikongwe nchini Tanzania


Picha: Mwili wa mchezaji wa Fiorentina ulivyowasili kanisani kupewa heshima ya mwisho

Mwili wa marehemu Davide Astori ambaye alikuwa mchezaji na kepteni wa Fiorentina, umeagwa leo na kupewa heshima za mwisho kwenye kanisa la Santa Croce church, Florence huku maelfu ya watu na mastaa mbali mbali wa soka wakihudhuria. Hapa nchini ni picha za mwili huo ulipowasilishwa kanisani hapo.









Simba SC ilinyimwa penati - Mwamuzi

Mwamuzi mkongwe mwenye beji ya FIFA nchini, Osman Kazi amesema kuwa Simba SC ilinyimwa penati ya wazi wakati wa mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC uliyopigwa uwanja wa Taifa licha ya vijana hao kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 0.
Mwamuzi Osman Kazi akichambua marudio ya michezo iliyopita
Kazi ambaye ni mwamuzi mstaafu na mwenye heshima kubwa nchini kufuatia kutenda vema kazi yake awapo uwanjani ameyasema hayo hapo jana kupitia luninga ya Azam tv.
Emmanuel Okwi alikuwa na mpira na anapo ingia nao eneo la goli, Ndikumana hajaugusa ule mpira bali mguu wake umeukwatua mguu wa kulia wa Okwi.
Kwa hiyo hii ilikuwa penati ya wazi kabisa, mwamuzi alikuwa karibu kabisa na eneo la tukio wala hakuitaji usaidizi wowote ila aliwanyima tu penati.
Mwamuzi Osman Kazi akiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Katika mchezo huo Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 5 – 0 dhidi ya Mbao FC huku beki wao Yusuph Ndikumana akitolewa kwa kadi nyekundu.


 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo