Showing posts with label Video. Show all posts
Showing posts with label Video. Show all posts

Utweve Makete: Serikali imetusaidiaje?

Mwenyekiti wa CCM tawi la Utweve Jeco Sanga amehoji Msaada wa serikali kwenye zahanati ya kijiji cha Utweve wakati wa kupokea utekelezaji wa ilani ya CCM 2016/2017 iliyosomwa kwao hii leo

Tazama video hiyo hapo chini


Lowassa aibuka na Hili, Hebu Msikilize




Rais Magufuli ataka kiongozi huyu afukuzwe kazi

Rais Dkt. John Magufuli ameagiza wataalamu wote wa idara za maji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hiyo na kuwawajibisha wahusika pale miradi isipotekelezwa

Tazama video hapa Chini:-


Sugu na Masonga "wametoroshwa" Gerezani - Mbowe

Kufuatia  kuachiwa huru kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga kutoka Gereza la Ruanda, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema bado hawajafahamu ni taratibu gani zimetumika kuwaachia huru wakati  kifungo chao kilikuwa bado.

“Katika mazingira ya kawaida, siku yao ya kifungo walichokuwa wamepewa kilikuwa kinaishia Juni 5, mwaka huu, lakini ghafla wakapewa taarifa kwamba wataachiwa leo. Hatuna hakika sana ni taratibu gani zimetumika kufupisha kifungo chao kwa sababu jambo hilo halijawekwa wazi.

“Tangu wamewekwa gerezani ni takribani miezi mitatu, mawakili wetu walifanya jitihada za kuhakikisha rufaa yao katika mazingira ya dharura inasikilizwa, lakini haikuwahi kupata jaji wala kusikilizwa kwa sababu kila jaji aliyepangiwa kesi hiyo alionekana ana udhuru,”alisema Mbowe.

Aidha, amesema wao wanaamini kesi hiyo haikuwa ya haki kwa sababu watuhumiwa walinyimwa dhamana mwanzoni, na kutokana na mazingira ya kesi yenyewe hawakutakiwa kupewa kifungo. 

Pia amedai kwamba wataendelea na rufaa yao ili kuweka rekodi sawa na kudhihirisha kwamba Sugu na Masonga hawakuwa na makosa.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao. Tazama Video hapo chini:-


Sugu Azungumza Baada ya Kuachiwa Kutoka Gerezani

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, amefunguka na kuweka wazi kilichojiri.

Amesema hakuwa anafahamu iwapo angeachiwa huru leo hadi polisi walipomfuata na kumwambia ajiandae. Amedai mapaka sasa hafahamu imekuwaje hadi akaachiwa kwani ilijulikana ataachiwa Juni 5, ambapo kifungo chake kingekamilika.

“Watu wote walitarajia ningetoka jela mwezi Juni, lakini ghafla jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi (leo) natakiwa niachiwe huru, nilipotoka nje nikakuta askari wengi, nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimi na mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maofisa magereza watano hadi nyumbani na kutukabidhi kwa familia.

“Watu wanauliza, imekuwaje? Lakini mimi ninawaambia sijui, kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place, utumishi uko palepale kwa level ileile, tulikuwa na exposure sasa hivi tumeongeza experience,” amesema Sugu.


Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Tazama zaidi kwa kubonyeza Play hapa Chini:-


Chama cha MDA chafanya Makubwa Makete



Chama cha Maendeleo Makete (MDA) jana kimekabidhi serikalini bati 150, mifuko 100 ya saruji pamoja na misumari Ya bati kilo 10 kwa ajili ya ujenzi wa bweni jipya la wavulana shule ya sekondari Mang'oto wilayani Makete mkoani Njombe
Tukio hilo limefanyika shuleni hapo ambapo Makamu mwenyekiti wa chama hicho Philipo Mahenge amesema mbali na Chama cha Maendeleo Makete kuguswa na tukio hilo pia waliwashirikisha wadau mbalimbali ambao nao wamechangia michango yao

Amesema hayo ni miongoni mwa malengo ya MDA kuleta maendeleo kwa wilaya ya Makete kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo, huku akiwapongeza wananchi wa kata ya Mang'oto na Makete kwa ujumla kwa hatua ambazo wamekwisha zichukua tangu tukio la moto lilipotokea shuleni hapo
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa bati hizo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Veronica Kessy ameshukuru kwa msaada huo na kuendelea kuikumbusha jamii kuwa Maendeleo yataletwa na watu
Mkuu huyo wa wilaya ameshukuru kwa umoja, mshikamano na ushirikiano mzuri uliopo ndani ya chama hicho ambao umewezesha upatikanaji wa vifaa hivyo kwani uamuzi huo wa wanamakete waishio nje ya Makete kupitia MDA umefanikisha jambo hilo
Awali akisoma taarifa ya hatua mbalimbali zilizofikiwa baada ya bweni hilo kuungua Machi 12 mwaka huu, Afisa mtendaji Kata ya Mang'oto Bw. Mengi Chalamila amesema, shilingi milioni sita laki saba sabini na tatu elfu, pamoja na michango mingine ya vifaa kutoka kwa wadau imewezesha ujenzi wa bweni jipya kuanza ambapo ujenzi huo kwa sasa umefikia hatua ya lenta
Nao wanafunzi wanaosoma shuleni hapo wamesema wanashukuru kwa misaada inayoendelea kutolewa baada ya bweni hilo kuungua kwa kuwa yote hayo ni kwa ajili ya wao kusoma katika mazingira mazuri
Baadhi ya wazazi waliozungumza na mwandishi wetu wamesema msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi huo ambao una umuhimu mkubwa katika elimu Diwani wa kata ya Mang'oto Mh Osmund Idawa amesema vifaa hivyo walivyokabidhiwa vitafanikisha kuharakisha ujenzi wa bweni hilo
Machi 12 mwaka huu bweni la wavualana katika shule ya sekondari Mang'oto liliteketea kwa moto ambapo ujenzi wa bweni jipya unaendelea na inatarajiwa litakamilika Juni Mwaka huu
Tazama video Hizi:-


Steve Nyerere amvua nguo aliyezaa na Masogange, adai alichangia kulia tu msibani

Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kutofikisha fedha za michango zilizobaki kwenye msiba wa Agness Masogange, na kusema kuwa pesa hizo haziwezi kupewa familia.

Steve Nyerere amesema kwamba pesa hizo ambazo zimetajwa kuwa milioni mbili zimekusudiwa kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, atakapoanza kidato cha kwanza hapo mwakani,

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba familia ya Agness inapaswa kushukuru kwa mchango wao walioutoa kumzika ndugu yao, na sio kuanza kuulizia masuala ya pesa, kwani pesa hizo si kwa ajili yao bali ni kwa ajili ya mtoto.


Mkandarasi aliyemchefua Rais Magufuli akamatwa

ZIKIWA  zimepita  siku sita   toka   Rais  Dkt  John  Magufuli  kuagiza  vyombo vya  ulinzi na  usalama  mkoa  wa  Iringa kuwakamata   aliyekuwa  mkuu wa  chuo   cha  elimu Mkwawa  Prof Pak Mushi na  mkandarasi  aliyehusika  katika  ujenzi  wa ukumbi  wa bilioni 8.8  katika  chuo cha Mkwawa Iringa ,tayari jeshi la  polisi mkoa  wa  Iringa  limemkamata  mkandarasi wa  ujenzi huo .

Wakizungumza na  waandishi  wa  habari jana  kamanda wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Juma  Bwire   na kamanda  wa  taasisi ya  kupambana na  rushwa  nchini (Takukuru ) Aidan  Ndomba walisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo  Godwin Mshana wa  kampuni ya  Engineering  Service  Ltd  mkazi wa Gangilonga  mjini hapa alikamatwa  toka   Mei  3 mwaka  huu ikiwa ni  siku moja  toka  Rais  alipotoa  agizo hilo .

" Kufuatia  agizo la  Rais  Dkt  Magufuli  kuhusu  ujenzi wa  ukumbi wa  mikutano chuo   kikuu cha  Mkwawa  uliojengwa   chini ya  kiwango  agizo  alilolitoa  wakati  akiwahutubia  wanajamii wa  chuo  hicho  tulifanya msako  mkali na  kufanikiwa  kumkamata  mtuhumiwa  huyo  akiwa nyumbani kwake Gangilonga  "A" "

Tazama Video Hii>>>>>>


Marufuku kunirekodi - Katibu wa CCM

Aahidi kuwashughulikia wanaomrekodi bila ridhaa yake, Tazama video hapo chini:-


Hata wao watakufa tu, msiogope kutekwa - CHADEMA

Ibrahim Ngogo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete amewaasa wanachama wake kutomfanyia MTU yeyote jambo baya hata awe wa CCM Pia ameongelea kuhusu kutekwa na kuwataka wanachama wake kutokuwa waoga kutetea maslahi ya taifa

tazama video Hii>>>>>>>>>>


Makubwa: Diwani aeleza anavyotafutwa anunuliwe

Diwani wa kata ya Matamba wilayani Makete mkoani Njombe Ephel Ng'ondya (CHADEMA) amesema amekuwa akipokea vishawishi vya kuhama kutoka kwa watu aliodai ni viongozi wa cha mapinduzi (CCM) Bila kuwataja majina kwa sasa, Diwani huyo amesema yeye ni dhahabu na ndiyo maana anasakamwa ili anunuliwe

Tazama Video hii>>>>>>


Kauli ya Mtoto wa Lowassa baada ya kumsikia Mwanadada akidai katelekezwa na Lowassa

Salaams. Nimesikia mwanamama mmioja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam. Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha. Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.
Fred Lowassa- Monduli
Video ya mwanadada akidai ni mtoto wa Lowasa


Aliyetelekezwa na Lowassa Huyu hapa, Afunguka Mazito


Adai yeye ni damu ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kabisa, ataka wapime DNA


DC: Ole wako Umpige Mkeo Uletwe Kwangu

Mkuu wa wilaya ya Iringa ametoa onyo Kali kwa wanaume wanaowapiga wake zao

Mkuu huyo wa Wilaya Richard Kasesela amesema ni marufuku kwa mwanaume kumpiga mkewe na endapo wakifikishwa kwake atawasweka ndani kwanza

Tazama video Hii:-


Kinyambe "aonekana" Mbarali Mbeya

Aonekana akichekesha watu


Uchawi: Nyoka 3 wakutwa Sokoni Mafinga

Wafanyabiashara wapagawa, hawajui la kufanya, wazihusisha na uchawi Credits kwa Oliver Motto


Amani ukiiacha mbali hufanikiwi - Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu akiiacha amani mbali hawezi kufanikiwa katika mambo yake


Magufuli amesema hayo leo April 8, 2018 alipopata nafasi ya kuzungumza na wananchi na waumini aliposhiriki Ibada ya Kumsimika Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha. 
"Napofungua maombolezo nakutana na neno 'AMANI' naomba ni nukuu tu sitaweza kusoma yote "ukijiweka mbali na amani nikasahau kufanikiwa" kwa hiyo amani ukiiacha mbali hufanikiwi katika tafsiri yangu siyo nzuri kama ile ya 'philosophy' wanazozijua hawa wazee. Lakini katika Zaburi ya 122 mstari wa saba inasema 'Amani na ikae ndani ya kuta zako na kufanikiwa ndani ya majumba yako". Nikaenda Zaburi mstari wa nane inasema "Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara kwa mara maana wewe bwana peke yako ndiye unijaliae kukaa salama, nilipoenda Zabari ya 34 mstari wa 14 inasema "Uache mabaya ukatende mema utafute amani, ukaifuatie"alisema Magufuli 
Rais Magufuli aliendelee kuhubiri amani kwa kuendelea kusoma masomo mbalimbali na vifungu mbalimbali kwenye vitabu vya dini ambavyo vimezungumzia masuala ya amani 
"Nilipoenda Zaburi ya 119 ambayo ni ndefu zaidi nikachukua mstari wa 168 inasema "Wana wa amani nyingi waipendayo sheria yako wala hawana la kuwakwaza, ukienda Zaburi ya 29 mstari wa 11 neno amani pia lipo linasema "Bwana atawapa watu wake nguvu bwana atawabariki watu wake kwa amani" alisema Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwapongeza maaskofu hao akiwepo askofu aliyemaliza muda wake pamoja na askofu Amani ambaye amesimikwa leo na kudai wamekuwa mstari wa mbele kupigania amani na kuhubiri juu ya amani.
Tazama video hii:-


Polisi Mkikuta bangi kamateni kijiji Kizima - Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapiga marufuku askari polisi kufyeka mashamba ya bhangi, kwani hiyo siyo kazi walioajiriwa kuifanya


Rais Magufuli ametoa marufuku hiyo leo alipokuwa akihutubia wananchi waliofika kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba za askari polisi mkoani Arusha,  zilizofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na kusema kwamba jambo hilo sio kazi yao.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba kazi ya kufyeka mashamba ya bhangi ni ya wenyewe wananchi wanaolima bhangi hizo, na iwapo hawatamkamata mhusika wa shamba, basi wasombe kijiji kizima kwenda kulifyeka.
“Ninyi hamkuajiriwa kwenda kufyeka mashamba ya bhangi, makamanda wako na maaskari wako, wasikate mashamba ya bangi, hawakuajiriwa kufyeka bhangi, tumieni njia za intelijensia wenu mtamshika tu, kama shamba lipo karibu na kijiji, shika kijiji kizima, wazee, wanawake, watoto, ndio wakafyeke hilo shamba la bhangi, ila IGP usiwatume maaskari wako kufyeka bhangi, mtaumwa nyoka mle, mna uniform nzuri msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bhangi, mimi nisingefyeka bhangi, wa kufyeka wapo”, amesema rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba kazi yao ni kuhakikisha nchi inakuwa salama, hivyo masuala kama hayo sio majukumu yao pia ni udhalilishaji kwa jeshi la polisi.
Mtazame kwenye video hii hapa chini:-


Shabiki wa Simba aliyetoa taulo kwenye goli la njombe mji afariki dunia

BREAKING NEWS
Taarifa isiyo rasmi Shabiki wa timu ya Simba mkoani Njombe alietoa kitaulo cha mlinda mlango wa timu ya Njombe Mji amekutwa amekufa nyumbani kwake mgenderwa leo huku sababu ya kifo hicho bado hakijafahamika.
Baada ya vurugu za kitaulo pale uwanjani Sabasaba juzi alikamatwa na polisi na kuachiwa jana.
Goli kipa wa Simba amepost kuonyesha kafariki, Tazma video hapo chini:_


Mbunge atikisa Bunge, Ni Kuhusu BAKWATA kupewa Ukumbi wa Bunge

Mbunge amehoji kwa nini Bakwata wamepewa Ukumbi Bungeni kufanya kikao chao, Tazama video hii hapa chini:-



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo