Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea goli kipa namba moja wa Simba ambaye sasa amejiunga na Taifa Stars Aisha Manula kutocheza leo katika timu ya Taifa dhidi ya Algeria
Manara amesema kuwa Manula leo hakuweza kushiriki katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Algeria ni kutokana na mchezaji huyo kupata jeraha siku ambayo Simba ilicheza na Al Masry.
"Golikipa namba moja nchini Aishi Manula kuwakosa Algeria baada ya kupata maumivu kidogo ya Enka..jeraha hilo dogo alilipata siku Simba ilipocheza na Al Masry. Nimethibitishiwa taarifa hizi na Tanzania One mwenyewe....tuendelee kuiombea Stars na kuomba afya njema kwa Aishi Manula" alisema Haji Manara
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi