Shabiki ambaye hakujulikana mara moja ameingia uwanjani kisha kukimbilia golini mwa mlinda mlango wa timu ya Njombe Mji, David Kisu na kuchukua taulo lililokuwa golini hapo kisha kukimbia nalo wakati timu hiyo ikicheza na Simba uwanja wa Sabasaba Njombe hii leo Shabiki huyo anayedhaniwa kuwa ni wa Simba, amelipora taulo hilo na kuruka uzio wa uwanja huo na kukimbia nalo hali iliyozua taharuki uwanjani hapo Shabiki huyo amekamatwa nje ya uwanja na kuanza kupokea kipigo kidogo kabla ya kuokolewa na askari polisi waliokuwa uwanjani hapo, huku taulo hilo likichomwa moto jambo ambalo limefanyika haraka kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na polisi Zaidi Tazama Video hii hapa chini:-
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube