Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Mlinzi wa Kanisa atoroka na milioni 29 za Sadaka

Mlinzi wa Kanisa la ACK All Saints Mountain View lililopo Kangemi nchini Kenya anadaiwa kutoweka na fedha za sadaka kiasi cha Ksh 1.5 ambazo ni takribani shilingi milioni 29 za Kitanzania.


Inadaiwa kuwa, fedha hizo zilikuwa zimechangishwa kama sadaka ili kusaidia maendeleo ya kanisa lakini mipango hiyo ikayeyuka baada ya mlinzi huyo kuvunja sehemu fedha hizo zilikohifadhiwa kisha kutokomea nazo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, mshukiwa huyo anadaiwa kuiba fedha hizo kutoka kwa madhabahu ya kanisa hilo.

“Wakati mzee wa kanisa John Wainanina na mweka hazina Elizabeth Njoki walipokwenda kanisani kuchukua pesa hizo leo asubuhi, walikuta milango ikiwa wazi, jambo ambalo sio la kawaida."

"Walipotazama kwa makini meza ya Bwana ambapo mkate na divai huwekwa, walishtuka kupata ikiwa imevurugwa na pesa zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye droo chini ya madhabahu hazipo!" DCI alisema.

Wazee hao wa kanisa walipiga ripoti kwa polisi ambao wameanzisha uchunguzi wa kumsaka mshukiwa.

Waumini wa kanisa hilo ambao walighadhabishwa na wizi huo walisikika wakitoa laana kwa mshukiwa huku wengine wakimtaka asamehewe iwapo atajitokeza na kutubu dhambi zake.


Mama atengwa na jamii kwa kuzaa watoto 11 wenye upofu

Mwanamke ameelezea kwa hisia kuhusu kutengwa na jamii na marafiki baada ya kuzaa watoto 11 na amabo wote ni vipofu.

Katika Makala ambayo yalipakiwa na blogu ya YouTube, mama huyo kwa jina Agnes Nespond alieleza kwamba baada ya muemwe kufariki kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, amekuwa akipitia ugumu kuwalewa watoto wake 11 amabo wote wana ulemavu wa macho.


Alisema kuwa watoto wote hao ambao wengine wameshakua watu wazima kanisa hawawezi kujitegemea kutokana na ulemavu wa macho amabo umewaweka chini ya uangalizi wake katika kumudu mahitaji yao yote kutoka kula, kunywa na mahitaji mengine ya msingi.


Alisema kwamba tatizo hilo lilikuwa likiwapata watoto wake mmoja baada ya mwingine na aliendelea kujitahidi kuzaa kwa tumaini kwamba angezaa mtoto angalau mmoja mwenye anaona lakini wote kumi na moja wakawa na tatizo lile lile.


Licha ya madaktari kumhakikishia kila mara kwamba watoto wake watakuwa wakamilifu, walikuwa vipofu kila wakati baada ya kuzaliwa. Alichukua jukumu la kuchimba mizizi ya historia yake ili kuangalia ikiwa ni suala la urithi. 


Hata hivyo, Nespondi hakuweza kupata kiini chochote katika familia yake kuhusu upofu, isipokuwa wanafamilia wake ambao walikuwa na matatizo ya macho kutokana na umri wao.


Nespond ambaye ni mkaazi katika kijiji kimoja nchini Kenya ambacho wazalishaji wa Makala hawakuweka wazi alisema kwamba alianza kushuku huenda kuna mkono wa ushirikina katika tatizo hilo kwa wanawe ambao alisema licha ya kuwa watu wazima, bado wanamtegemea kutokana na kwamba hakuna mtu anayeweza kuwapa kazi.


“Kula ni shinda, kunywa ni shida sina mtu wa kunisaidia. Ni mimi tu peke yangu,” Nespond alieleza.



Mkuu wa shule atuhumiwa kubaka mwanafunzi

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mosa Mixed, iliyopo Wilaya ya Kisasi nchini Kenya, Bwana Samuel Kimanzi (58) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kitui kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule yake

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, mtuhumiwa amepandishwa kizimbanbi leo Juni 6, 2018 na kuongeza kuwa tukio hilo la ubakaji limetokea katika shule hiyo wakati mkuu huyo wa shule alienda katika bweni la wanafunzi wa kike usiku wa Mei 21, 2018 kwa lengo la kufanya ukaguzi wa kushtukiza.
Mwanafunzi aliyebakwa alidai kwamba siku ya tukio Bwana Kimanzi, alimtoa nje ya bweni na kumpeleka katika ukuta wa shule na kisha kumbaka na kuongeza kuwa alipewa vitisho endapo angetoa taarifa za tukio hilo.
Baada ya kuripoti tukio hilo kwa wanafunzi wenzake alichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa Kitui kwa matibabu ya dharura kabla ya kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi cha Mbitini Market akiwa na walezi wake
Kesi hiyo imetajwa kuendelea tena Septemba 3, 2018 ambapo upande wa mashtaka umepanga kuandaa mashahidi 10.
Mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilsha masharti ya kutoa pesa taslimu kiasi cha shilingi za Kenya 50, 000.


Biblia na Qur'an Tukufu kutozwa kodi

Serikali ya Uganda imeagiza kuanzia sasa vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran vinavyoingizwa nchini humo vilipiwe kodi

Viongozi wa Kidini kutoka madhehebu hayo mawili makubwa nchini humo wamepokea uamuzi huo kwa tahadhari kubwa na mshangao huku wakisisitiza kwamba, vitabu hivyo vya kidini havipaswi kutozwa kodi kwani vinatumika kujenga na kuimarisha imani za kiroho za wananchi wa Uganda.
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Nchini Uganda, Ramadhan Mugalu, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa, hatua hiyo imevuka mipaka, na kuhoji inawezaje kutoza kodi neno la Mungu?
Kwa upande wake Kamishna wa Makanisa nchini humo, Mchungaji Joram Kahenano, amesema Kanisa lake litalazimika kuongeza bei ya Biblia moja kutoka shilingi za Uganda elfu tatu hadi elfu 18 ili kufidia gharama za kodi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, uamuzi huo umetolewa baada ya miezi kadhaa ya majadiliano kati ya Mamlaka ya Kodi na Taasisi za Kidini.


Mwanamke auawa kwa kulazimisha kufunga ndoa

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Samuel Bariluno katika kijiji cha Nakwaya, wilaya ya Mityana chini Uganda amemuua kwa bastola mchumba wake kwa kile kinachosemekana kuchoshwa na tabia ya mwanamke huyo kukumbushia mara kwa mara suala la kufunga ndoa

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majirani wanasema wawili hao walikua wanatabia ya kugombana mara kwa mara kutokana na marehemu aliyejulikana kwa jina la Agnes Nakimera kutilia msisitizo suala la kufunga ndo na bwana bariluno.
Mashuhuda wanasema kwamba bwana Bariluno ambaye ni mfanyabiashra katika soko la Wakiseka, alimpiga risasi mchumba wake huyo kisha nayeye kutaka kujiua kwa bastola hiyo lakini ilishindikana na badala yake alipata majeraha.
Watoto wa familia hiyo wamesema kwamba wazazi wao walikua wanagalia runinga kabla ya kuanza kujibizana kwa sauti na ndipo walipomuona baba yao akichukua  bastola na kumfyatulia mama yao.
“Baba alichukua bastola na kumfyatulia mama kifuani na baada ya kugundua mama yupo katika hali mbaya akaamua kujiga risasi na kujijeruhi vibaya” alisema mmoja wa watoto wa familia hiyo.
Marehemu Agnes Nakimera alifariki dunia katika kituo cha afya cha Bukomero.
Mkuu wa polisi wa katika wilaya ya Mityana Kamanda John Bosco Serunjoji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wanamshikilia mtuhumiwa ambaye anatibiwa katika Hospitali ya Rufaa Mulango.


Bwawa laua watu 27

Watu takribani 27 wamefariki dunia huku maelfu ya watu wakikosa makazi baada ya bwawa kubwa lililoko mjini Nakuru nchini Kenya kuvunja kuta zake siku ya Jumatano usiku.
Juhudi za ukoaji zinaendelea kufanywa na maafisa wa msalaba mwekundu wakisaidiana na vijana wa huduma za kitaifa.


Hizi Ndio Nchi zinazowanyanyasa waandishi wa Habari Duniani

DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI ya Marekani imetaja nchi tisa duniani ikidai zinanyanyasa vyombo vya habari na waandishi wa habari na kutoa wito kwa dunia kuruhusu uhuru wa maoni na utawala wa demokrasia

Akizungumza juzi na waandishi wa habari jijini Washington DC nchini humo, Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Heather Nauert alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Cambodia na Ufilipino akisema zimekuwa na matukio ya kufungia vyombo vya habari.
Alizitaja pia nchi za Afghanistan, Burma, Cuba, Uturuki, Misri na China kwa unyanyasaji wa waandishi wa habari.
“Waandishi wa habari wanakamatwa kutokana na kazi zao katika maeneo ya Burma, Uturuki, Misri na China. Wanafamilia nao wamekuwa wakikamatwa kutokana na kazi za ndugu zao,” alisema na kuongeza: “Mifano hii inaonyesha jinsi usalama na uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vya habari na mazingira yao wanavyotishiwa. Tungependa kusisitiza umuhimu wa usawa na uwepo wa demokrasia ya wazi na uhuru wa maoni.”
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ndiye msemaji mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas hakupatikana kuzungumzia madai hayo kwani simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokewa. Pia, ujumbe wa maandishi kwa simu aliotumiwa haukujibiwa.
Mbali na Dkt Abbas, pia Waziri wa Habari, Dkt Harrison Mwakyembe na msaidizi wake, Juliana Shonza hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Kauli hiyo ya Marekani ilitolewa Mei 3, 2018, katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo hapa nchini, wadau wa habari waligusia matukio ya utekaji wanahabari, kufungiwa vyombo vya habari na kutozwa faini kubwa kwa vyombo hivyo.
Mwandishi kutoweka
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma, suala la kutoweka kwa mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Azory Gwanda nalo lilichukua nafasi kubwa.
Azory aliyekuwa akifanya kazi wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani alichukuliwa na watu wasiojulikana wakiwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser Novemba 2017 na hajaonekana hadi leo.
Miongoni mwa taasisi zilizotoa matamko ni pamoja na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa- Tan), Muungano wa Klabu za Habari Tanzania (UTPC), Bazara la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Hata hivyo, Dkt Mwakyembe alisema Serikali imefungua milango ya majadiliano na wanahabari kuhusu changamoto zao.
Alisema ingawa Serikali imetoa haki ya kupelekwa mahakamani mashauri kuhusu sheria ambazo zimepitishwa, bado kuna fursa nzuri ya kufanya mazungumzo miongoni mwa wadau.

Chanzo: Swahilihub


Mbaroni kwa Kusajili Namba ya simu ya Mbunge

MWANAMUME anayeshtakiwa kwa madai ya kusajili nambari ya simu ya Mbunge mwakilishi wa wanawake kaunti ya Murang’a Kenya Bi Sabina Chege na kuitumia kuwapunja wabunge wengine pesa angali rumande baada ya kushindwa kupata dhamana ya Sh1 milioni.
Wazir Benson Masubo Chacha aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni pesa taslimu wiki iliyopita na ameshindwa kupata pesa hizo.

Hakimu mkuu Bi Roseline Oganyo wa mahakama ya Citi aliamuru mshtakiwa awasilisha mdhamini wa Sh3milioni ikiwa atashindwa kupata dhamana hiyo.
Bw Chacha almaarufu Sabina Chege aliyetiwa nguvuni nchini Tanzania amekaa rumande kwa zaidi ya siku 40. Alipewa dhamana hiyo baada ya afisa wa urekebishaji tabia Bi Javenine Akinyi kuwasilisha ripoti kutoka kwa familia ya mshtakiwa ikiiomba korti imwachilie kwa dhamana.
Katika afidaviti iliyowasilishwa kortini  na Inspekta John Kiprop kutoka kituo cha Polisi kilichoko Bungeni ilidaiwa Bw Masubo alitiwa nguvuni  eneo la Tarime nchini Tanzania akipania kutorokea nchini DRC
Wiki iliyopita, mahakama ilikuwa imetoa kibali cha kumtia nguvuni Bw Masubo kushtakiwa kwa makosa ya kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.
Bi Njagi alifahamishwa kuwa mshukiwa huyo alitiwa nguvuni mnamo Machi 30, 2018 na polisi hawakuwa na muda wa kutosha kumhoji na kuandika taarifa kutoka kwa mashahidi ambao wengi ni wabunge wanawake.
“Naomba hii mahakama imzuilie mshtakiwa katika kituo cha polisi kumhoji na pia taarifa ziandikishwe kutoka kwa Bi Chege na walalamishi wengine aliojaribu kupokea pesa kutoka kwao akitumia jina la mbunge huyo,” akaomba Bw Kiprop.
Wakili Job Ngeresa anayemtetea Bw Masubo alipinga ombi hilo la kuzuiliwa kwa muda wa siku saba.
“Mshukiwa alikamatwa Machi 30, 2018 na amekuwa mikononi mwa polisi,” akasema na kuomba mshukiwa aachiliwe kwa dhamana ili aweze kuenda hospitali kutibiwa, kwa vile anaugua maradhi ya ubongo yajulikanayo kwa lugha ya Kiingereza -Migrane.
“Mshukiwa huyu hakuwa akitoroka mbali alikuwa anaenda hospitali ya Muimbili iliyoko mjini Dar-es-Salaam kupokea matibabu ya kichwa. Mara kwa mara amekuwa akienda nchini Tanzania kusaka tiba ya kichwa kwa vile anapoanza kuugua yeye hutoa nguo akaachwa uchi wa mnyama,” Bw Ngeresa alimweleza hakimu.
Wakili Job Ngeresa atawasilisha ombi katika mahakama kuu akiomba dhamana hiyo ipunguzwe.


Mtoto akutwa na sindano 7 tumboni

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti ya Pokot amekutwa na sindano 7 za kushonea kwa mkono tumboni mwake, baada ya kupigwa picha ya xray

Mtoto huyo alipelekwa hospitali ya Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu ya maumivu ya tumbo ambayo alikuwa akiyapata kwa muda mrefu bila kujua tatizo ni nini.
Bibi yake Bi. Emily Linga'a ambaye ndiye anayeishi naye, amesema mtoto huyo alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawakuweza kubaini mara moja chanzo cha maumivu hayo na kuendelea kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini baada ya kuona anazidi kualalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana tatizo hilo.
“Kwanza nilidhani mtoto alikuwa na minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana sindano tumboni mwake, nilikuwa nahisi ni malaria siku zote na kumpa dawa za maumivu”, amesema bibi huyo ambaye anaishi naye, baada ya mama yake kumuacha alipoolewa na mwanaume mwengine.
Madaktari wa hospitali hiyo wamempa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili kuwea kufanyiwa upasuaji wa tumbo, na kutolewa sindano hizo ambazo hazijajulikana zimeingiaje.


Daktari awapa wanawake Dawa Feki

Mwanamke mmoja Guinea ambaye aliwauzia dawa za kienyeji kwa wagumba, akiwaambia kuwa wangepata mimba, amefungiwa miaka mitano.
N'na Fanta Camara alitengeneza dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha matumbo yao kufura na kuonekana kuwa ni wajawazito.
Daktari huyo wa kienyeji anasemekana kuwalaghai zaidi ya wanawake 700 akiwa toza fedha nyingi kwa matibabu.
Mwandishi wa BBC Alhassan Sillah aliyopo jiji la Conakry , anasema waathirika waliojitokeza mahakamani walikasirika kwamba hakupata hukumu nzito.
Camara,alipatwa na hatia ya kumuiga daktari kwa kuwapatia wanawake hao dawa zilizowadhuru na zilizoweka maisha yao hatarini.
Aliagizwa kulipa fidia ya dola za Marekani 165,000
Washirika wengine wawili walihukumiwa kwa mashtaka hayo pia na kuhukumiwa kifungo cha muda wa miaka tatu hadi minne gerezani.
Kutokana na huduma hizo wagonjwa walilipa dola 33 kwenye nchi ambayo kipato cha kila mwezi kinakadiriwa kuwa dola 48.
Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.
Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji.
chanzo:BBC


Mwanafunzi kidato cha kwanza abaka na kuua

Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Gituto katika kaunti ya Murang'a nchini Kenya, ameuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kubainika kumbaka binti mwenye umri wa miaka 12 na kisha kumnyonga

Dada wa binti aliyeuawa Grace Kabura, amesema alimuacha mdogo wake nyumbani, na aliporudi hakumkuta.
“Nilirudi nyumbani sikumkuta Wambui, nikawauliza watoto waliokuwa wakicheza jirani wakaniambia ameondoka na Duncan Wakahiu”, amesema dada wa binti huyo aliyeuawa.
Grace ameendelea kwa kueleza kwamba baada ya hapo aliwaomba watoto wamuonyeshe nyumbani kwa kijana huyo na kuwakuta wazazi wake, kisha akawaeleza kuwa anamtafuta mdogo wake ambaye ameonekana kuelekea hapo.
Baada ya hapo wazazi wa kijana wakamuita mtoto wao na kumuuliza mahali alipo mwenzake, akawaambia amemtuma dukani na hajarudi.
Grace ameendelea kueleza kuwa wazazi wake waliingiwa na mashaka na kuamua kupekua ndani ya chumba cha kijana wao, na kukuta mwili wa Wambui ukiwa uvunguni na kijana huyo kukimbia.
Hata hivyo wananchi waliamua kumsaka kijana huyo na walipompata walimshushia kipigo na kumuua.


Anusurika kufa baada ya kumeza mswaki

Mtu mmoja nchini Kenya amefanyiwa upasuaji wa kisasa wa kutoa mswaki, aliokuwa ameumeza kwa bahati mbaya wakati akisafisha kinywa

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la David Charo mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Ganze Kaunti ya Kilifi, alimeza mswaki wakati akisafisha kinywa kujiandaa kunywa chai, tukio lililomsababishia ahisi kama ndio utakuwa mwisho wa uhai wake.
“Nilikuwa najitayarisha kupiga mswaki ndio nikunywe chai halafu nianze safari yangu ya kuja Mombasa. Kupiga mswaki hivi, kwa bahati mbaya ule mswaki ukateleza na ukaingia ndani”, amesema David.
Hata hivyo madaktari wa hospitali kuu ya Coast walifanikiwa kuutoa mswaki huo kwa njia ya kisasa bila kumfanyia upasuaji, na kuokoa maisha yakje.
Imeelezwa kwamba iwapo madaktari hao wangeshindwa kuutoa kwa njia hiyo, wangelazimika kumpasua tumbo ii kuutoa mswaki ambao tayari ulikuwa umeanza kumletea madhara kiafya.


Mbunge ataka wanaume kuoa wake wengi

Mbunge mmoja nchini Kenya ameibua hoja kuwataka wanaume kuoa wanawake wengi, ili kuweza kusaidia malezi ya familia na kupunguza watoto wa mitaani

Mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Gathoni wa Muchomba kutoka kaunti ya Kiambu, amesema ameona ni vyema iwapo wanaume wataoa wanawake wengi kwani watoto wengi nchini humo wamekuwa wakilelewa na mzazi mmoja, jambo ambalo linasababisha malezi mabaya na watoto kuangukia kwenye matatizo.
“Nimetoa haya matamshi kama kiongozi wa Kiambu kwa sababu ya matatizo ambayo tunayo ya watoto kulelewa na 'single mother', nadhani hilo linaweza likawa suluhisho litasaidia kwenye malezi ya familia, kama uko na uwezo wa kutunza na kutumikia kwa mahitaji yake yote, naona tumekuwa tunaacha yale ambayo tulikuwa tunafuatilia miaka iliyopita”, amesema Mbunge huyo.
Mbunge huyo amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.
Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.


VIDEO: Askofu avamiwa Akiendesha ibaada ya Pasaka

Askofu Wilberforce Kityo Luwalira amenusurika shambulizi dhidi yake katika Ibada ya Pasaka hapo jana katika Kanisa la Mt. Paulo huko Namirembe Uganda

Angalia video hapo chini-


Mchungaji akamatwa na Polisi akijaribu kumfufua Marehemu

Mchungaji mmoja  nchini  Msumbiji amejikuta akiishia  mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio.

Mchungaji huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali inayofahamika kwa jina Chimoio iliyopo katika jimbo la Manica, ili akafanye muujiza ambao alidai ana uwezo wa kufanya na alipowashawishi Maafisa wa hospitali walimruhusu aingie ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti ili atekeleze muujiza huo.

Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi, hakuweza kurejesha uhai wa marehemu na familia hiyo haikushangazwa na kushindwa kwake.

Dada wa marehemu  ambaye hakutaka jina lake litajwe aliwaambia waandishi wa habari kuwa “Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.

“Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja kasisi alipaza sauti akisema, ‘amka, kijana wa Mungu!, Hatukuamini angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.

“Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu." 
Alisema  Dada wa Marehemu


Mrembo aliyeruka kutoka ghorofa ya sita akimkimbia mbakaji atupwa jela

Mwanamke mmoja mjini Dubai amejikuta akiishia jela baada ya kuuguza majeraha aliyoyapata wakati akimkimbia mbakaji kwa kuruka nje ya chumba cha hoteli kilichokuwa ghorofa ya sita

Ekaterina Stetsyuk
Mrembo huyo aitwaye Ekaterina Stetsyuk (22) ambaye kazi yake ni Mwanamitindo amesema alipatana na mwanaume mmoja mwenye uraia wa Pakistani ambaye ni mfanyabiashara wa vipodozi kuwa wakutane Dubai kwa ajili ya mazungumzo ya kumtangazia bidhaa zake.
Ekaterina kutoka Urusi amesema kuwa siku ya kwanza walipokutana katika Appartment hiyo ambayo mfanyabiashara huyo alikuwa amepangisha walizungumza kwa ufupi na baadaye kuanza kupata vinywaji.Mama mzazi wa Ekaterina ‘Inga’ amesema baada ya mfanyabiashara huyo kulewa alimpeleka hadi chumbani kwake ambapo alianza kumfosi kushiriki tendo la ndoa huku akimtishia kumuua.
Bi. Inga akizungumza na gazeti la Vatan wa Urusi amesema kuwa mwanaye aliamriwa avue nguo na mwanaume huyo ambaye alimwambia kuwa ana miaka 39 ,na alipokataa kufanya hivyo mwanaume huyo alimshikia kisu kutishia kumuua.Amesema baada ya purukushani Ekaterina alifanikiwa kumuangusha mwanaume huyo na ndipo alipopata mwanya wa kufungua dirisha na kuruka nje ambapo Polisi mjini Dubai wameeleza kuwa chumba hicho kilikuwa ghorofa ya sita.
Tulipigiwa simu na ubalozi wetu (Ubalozi wa Urusi) kuwa mtoto wetu amepata ajali ikabidi tuulize kilichomsibu lakini hatukupewa taarifa kamili hadi tuliposafiri kwenda Dubai,“ameendelea kusema Bi. Inda.
Kwa bahati nzuri tulimkuta anauwezo wa kuongea lakini alikuwa anashindwa kukaa, alitueleza kilichomsibu kuwa alikimbia mtu aliyekuwa anataka kumbaka, ambaye sisi alitutaarifu kuwa ni rafiki yake kibiashara,“amesema Inda.
Akitoa ushuhuda wa tukio hilo kwenye mahojiano na Polisi mjini Dubai Machi 21, 2018. Ekaterina amesema kuwa alishikiwa kisu na mwanaume huyo akimtaka avue nguo zote kitu ambacho alikataa katu.
Baada ya hapo ndipo alipoanza kuvutwa nywele kitu ambacho kilipelekea purukushani na akafanikiwa kumpokonya kisu mwanaume huyo.
Ekateria amesema alipofanikiwa kuchukua kisu mwanaume huyo alienda kufunga mlango huku akiambiwa kuwa ataletewa wanaume wambake endapo atajifanya jeuri, kauli ambayo ilimfanya akimbie kwa kutokea dirishani.
Polisi mjini Dubai wamesema siku ya tukio mwanaume huyo (Mfanyabiashara) alienda polisi kutoa taarifa kuwa amevamiwa na mwanamke akiwa kwenye chumba chake kwa kuchomwa kisu. Na kwenye taarifa yake alidai kuwa mwanamke huyo walikuwa wamepanga kufanya naye biashara na baada ya tukio hilo hakujua alipokimbilia.
Licha ya maelezo yote mawili, Eketarina ameshikiliwa na jeshi la polisi mjini Dubai kwa tuhuma za kujeruhi na kutaka kuuwa.
Eketerina amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye paja na mgongoni ambapo ndiyo maeneo yanayoripotiwa kuwa aliumia zaidi kwenye ajali hiyo.
Wazazi wa msichana huyo wamesema kuwa mtoto wao alikutana na mwanaume huyo kwa njia ya mtandao wa Instagram kabla ya kujenga mahusiano ya kibiashara.
Chanzo: Gazeti la Vatan


Mamba avamia hospitali, ahusishwa na ushirikina

Mamba amesababisha taharuki katika hospitali ya mji wenye migodi ya dhahabu wa Hwange nchini Zimbabwe.
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne jioni wiki hii ambapo dereva wa taxi alikuwa wa kwanza kumuona mamba huyo na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama.
“Ndani ya dakika tano nilipokea takribani simu 10 za wakaazi wa eneo hilo waliokuwa kwenye taharuki kubwa,” Afisa mwandamizi wa bodi ya makaazi, Themba Tshuma anakaririwa.
“Mengi yamezungumzwa na wakaazi wa eneo hilo waliokuwa hawaamini wanachokiona. Wengine wamehusisha na ushirikana, wamedai kuwa inawezekana alikuwa ni mtu mshirikina ambaye alishindwa kufuata masharti na kujikuta anageuka kuwa mamba,” aliongeza.
Gazeti la The Chronicle limeeleza kuwa mamba huyo alikaa katika geti la hospitali hiyo na kutishia kumshambulia mtu yeyote aliyesogelea geti. Hata hivyo, maafisa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Zimbabwe walifika na kumuua mamba huyo.
Haijafahamika rasmi alikotokea mamba huyo kwani chanzo kikubwa cha maji kiko umbali wa kilometa kumi kutoka kwenye mji huo.


Amzika mtoto wake akiwa hai

Polisi wa Migori nchini Kenya wanachunguza kifo cha mtoto mwenye umri wa miezi 6, ambaye inasemekeana alifukiwa akiwa hai na baba yake mzazi

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Chief Fredrick Owino, mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Marcellus Odek, alirudi nyumbani kwake akiwa amelewa na kuchukua jembe na kuchimba kaburi, ambalo alimzika mtoto huyo ambaye ameelezwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupumua.
Taarifa zaidi zinasema kwamba mama wa mtoto huyo Annah Auma wakati tukio linatokea alikuwa amepoteza fahamu kutokana na tatizo la kifafa alilokuwa nalo, na alifanya tukio hilo mbele ya familia yake na majirani, usiku wa Machi 14 mwaka huu.
Ndugu wa familia hiyo Milicent Achieng amesema mtuhumiwa aliwakuta nyumbani na moto akiwa anapumua, kabla hjaanza kuchimba kaburi na kumfukia, na alipoomba msaada kwa watu walikataa nakumshauri akimbie kwani huenda angemuua na yeye.


Picha: Mvua zasababisha madhara, Magari yaangukiwa na Miti

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini Kenya zimeleta madhara ikiwemo miti kuangukia magari katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kama inavyoonekana katika picha hizi


Abiria wachoma moto basi walilosafiria

Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mombasa kwenda Nairobi nchini Kenya, wamelichoma basi walilokuwa wakisafiria katika eneo la Tajmali huko Embakasi

Chanzo cha abiria hao kufanya hivyo kimeelezwa kuwa ni hasira walizokuwa nazo baada ya dereva kulazimisha kutumia njia ambayo imeathirika na mafuriko, na kuhofia kukaa njiani kwa muda mrefu kutokana na foleni.
Abiria hao walikuwa wakimtaka dereva kutumia njia ya kupitia Outering kwenda Nairobi, badala ya barabara ya Mombasa ambayo dereva alikuwa akisisitiza kuitumia.
Baada ya mvutano wa hapa na pale ndipo abiria hao waliposhikwa na hasira na kuamua kulichoma moto basi hilo na kisha wote kukimbia, na dereva naye kuamua kukimbia eneo la tukio.
Source
Ghetto Radio Kenya
Basi lililochomwa moto na abiria


 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo