Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kutoa ahadi kuwa endapo klabu ya Liverpool itaifunga klabu ya Manchester United leo basi yeye atahama CCM na kuhamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA)
Haji Manara ametoa ahadi hiyo leo dakika kadhaa kabla ya klabu hizo kushuka dimbani katika uwanja wa Old Trafford huku klabu yake hiyo pendwa ya Manchester United ikiwa nyumbani.
"Ikitokea Liverpool kuifunga Manchester nahama CCM najiunga na chama cha Hashim Rungwe ..hawatufungi hata kwa bahati mbaya" alisema Haji Manara
Haji Manara ni mwanachama mzuri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kushika nyazifa mbalimbali ndani ya chama hicho kikongwe nchini Tanzania
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi