Bei ya nyama yapanda Morogoro baada ya machinjio ya manispaa kuhamishwa

Bei ya nyama katika manispaa ya Morogoro imepanda kutoka shilingi elfu tano hadi shilingi elfu saba kwa kilo kufuatia mamlaka ya chakula na dawa TFDA kufunga machinjio ya manispaa hiyo na kuyahamishi Dakawa wilayani Mvomero.

Wakizungumza  nasi kwa nyakati tofauti wafanyabiashara wa nyama wameeleza kusikitishwa na kitendo cha manispaa ya Morogoro kushindwa kufanya ukarabati wa machinjio hayo kwa haraka hali inayosababisha bei ya nyama kupanda kwa kasi na kuwaumiza walaji ambapo wamesema kupanda kwa bei ya nyama ni kutokana na kuongezeka maradufu gharama za usafilishaji na ushuru katika machinjio ya Dakawa Mvomero.
 
Nao wateja wa nyama wakiwemo mamalishe na walaji wengine wamelalamikia manispaa ya Morogoro kushindwa kushughulikia tatizo hilo haraka huku wananchi wakishindwa kununua kitoweo hicho kutokana na bei  kupanda ghafla.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo