ZIKIWA zimepita siku sita toka Rais Dkt John Magufuli kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa kuwakamata aliyekuwa mkuu wa chuo cha elimu Mkwawa Prof Pak Mushi na mkandarasi aliyehusika katika ujenzi wa ukumbi wa bilioni 8.8 katika chuo cha Mkwawa Iringa ,tayari jeshi la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mkandarasi wa ujenzi huo .
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire na kamanda wa taasisi ya kupambana na rushwa nchini (Takukuru ) Aidan Ndomba walisema kuwa mtuhumiwa huyo Godwin Mshana wa kampuni ya Engineering Service Ltd mkazi wa Gangilonga mjini hapa alikamatwa toka Mei 3 mwaka huu ikiwa ni siku moja toka Rais alipotoa agizo hilo .
" Kufuatia agizo la Rais Dkt Magufuli kuhusu ujenzi wa ukumbi wa mikutano chuo kikuu cha Mkwawa uliojengwa chini ya kiwango agizo alilolitoa wakati akiwahutubia wanajamii wa chuo hicho tulifanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa nyumbani kwake Gangilonga "A" "
Tazama Video Hii>>>>>>