
Magufuli amesema hayo leo April 8, 2018 alipopata nafasi ya kuzungumza na wananchi na waumini aliposhiriki Ibada ya Kumsimika Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha.
"Napofungua maombolezo nakutana na neno 'AMANI' naomba ni nukuu tu sitaweza kusoma yote "ukijiweka mbali na amani nikasahau kufanikiwa" kwa hiyo amani ukiiacha mbali hufanikiwi katika tafsiri yangu siyo nzuri kama ile ya 'philosophy' wanazozijua hawa wazee. Lakini katika Zaburi ya 122 mstari wa saba inasema 'Amani na ikae ndani ya kuta zako na kufanikiwa ndani ya majumba yako". Nikaenda Zaburi mstari wa nane inasema "Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara kwa mara maana wewe bwana peke yako ndiye unijaliae kukaa salama, nilipoenda Zabari ya 34 mstari wa 14 inasema "Uache mabaya ukatende mema utafute amani, ukaifuatie"alisema Magufuli
Rais Magufuli aliendelee kuhubiri amani kwa kuendelea kusoma masomo mbalimbali na vifungu mbalimbali kwenye vitabu vya dini ambavyo vimezungumzia masuala ya amani
"Nilipoenda Zaburi ya 119 ambayo ni ndefu zaidi nikachukua mstari wa 168 inasema "Wana wa amani nyingi waipendayo sheria yako wala hawana la kuwakwaza, ukienda Zaburi ya 29 mstari wa 11 neno amani pia lipo linasema "Bwana atawapa watu wake nguvu bwana atawabariki watu wake kwa amani" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwapongeza maaskofu hao akiwepo askofu aliyemaliza muda wake pamoja na askofu Amani ambaye amesimikwa leo na kudai wamekuwa mstari wa mbele kupigania amani na kuhubiri juu ya amani.
Tazama video hii:-