Mbaroni kwa Kusajili Namba ya simu ya Mbunge

MWANAMUME anayeshtakiwa kwa madai ya kusajili nambari ya simu ya Mbunge mwakilishi wa wanawake kaunti ya Murang’a Kenya Bi Sabina Chege na kuitumia kuwapunja wabunge wengine pesa angali rumande baada ya kushindwa kupata dhamana ya Sh1 milioni.
Wazir Benson Masubo Chacha aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni pesa taslimu wiki iliyopita na ameshindwa kupata pesa hizo.

Hakimu mkuu Bi Roseline Oganyo wa mahakama ya Citi aliamuru mshtakiwa awasilisha mdhamini wa Sh3milioni ikiwa atashindwa kupata dhamana hiyo.
Bw Chacha almaarufu Sabina Chege aliyetiwa nguvuni nchini Tanzania amekaa rumande kwa zaidi ya siku 40. Alipewa dhamana hiyo baada ya afisa wa urekebishaji tabia Bi Javenine Akinyi kuwasilisha ripoti kutoka kwa familia ya mshtakiwa ikiiomba korti imwachilie kwa dhamana.
Katika afidaviti iliyowasilishwa kortini  na Inspekta John Kiprop kutoka kituo cha Polisi kilichoko Bungeni ilidaiwa Bw Masubo alitiwa nguvuni  eneo la Tarime nchini Tanzania akipania kutorokea nchini DRC
Wiki iliyopita, mahakama ilikuwa imetoa kibali cha kumtia nguvuni Bw Masubo kushtakiwa kwa makosa ya kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.
Bi Njagi alifahamishwa kuwa mshukiwa huyo alitiwa nguvuni mnamo Machi 30, 2018 na polisi hawakuwa na muda wa kutosha kumhoji na kuandika taarifa kutoka kwa mashahidi ambao wengi ni wabunge wanawake.
“Naomba hii mahakama imzuilie mshtakiwa katika kituo cha polisi kumhoji na pia taarifa ziandikishwe kutoka kwa Bi Chege na walalamishi wengine aliojaribu kupokea pesa kutoka kwao akitumia jina la mbunge huyo,” akaomba Bw Kiprop.
Wakili Job Ngeresa anayemtetea Bw Masubo alipinga ombi hilo la kuzuiliwa kwa muda wa siku saba.
“Mshukiwa alikamatwa Machi 30, 2018 na amekuwa mikononi mwa polisi,” akasema na kuomba mshukiwa aachiliwe kwa dhamana ili aweze kuenda hospitali kutibiwa, kwa vile anaugua maradhi ya ubongo yajulikanayo kwa lugha ya Kiingereza -Migrane.
“Mshukiwa huyu hakuwa akitoroka mbali alikuwa anaenda hospitali ya Muimbili iliyoko mjini Dar-es-Salaam kupokea matibabu ya kichwa. Mara kwa mara amekuwa akienda nchini Tanzania kusaka tiba ya kichwa kwa vile anapoanza kuugua yeye hutoa nguo akaachwa uchi wa mnyama,” Bw Ngeresa alimweleza hakimu.
Wakili Job Ngeresa atawasilisha ombi katika mahakama kuu akiomba dhamana hiyo ipunguzwe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo