Mwanamke ameelezea kwa hisia kuhusu kutengwa na jamii na marafiki baada ya kuzaa watoto 11 na amabo wote ni vipofu.
Alisema kuwa watoto wote hao ambao wengine wameshakua watu wazima kanisa hawawezi kujitegemea kutokana na ulemavu wa macho amabo umewaweka chini ya uangalizi wake katika kumudu mahitaji yao yote kutoka kula, kunywa na mahitaji mengine ya msingi.
Alisema kwamba tatizo hilo lilikuwa likiwapata watoto wake mmoja baada ya mwingine na aliendelea kujitahidi kuzaa kwa tumaini kwamba angezaa mtoto angalau mmoja mwenye anaona lakini wote kumi na moja wakawa na tatizo lile lile.
Licha ya madaktari kumhakikishia kila mara kwamba watoto wake watakuwa wakamilifu, walikuwa vipofu kila wakati baada ya kuzaliwa. Alichukua jukumu la kuchimba mizizi ya historia yake ili kuangalia ikiwa ni suala la urithi.
Hata hivyo, Nespondi hakuweza kupata kiini chochote katika familia yake kuhusu upofu, isipokuwa wanafamilia wake ambao walikuwa na matatizo ya macho kutokana na umri wao.
Nespond ambaye ni mkaazi katika kijiji kimoja nchini Kenya ambacho wazalishaji wa Makala hawakuweka wazi alisema kwamba alianza kushuku huenda kuna mkono wa ushirikina katika tatizo hilo kwa wanawe ambao alisema licha ya kuwa watu wazima, bado wanamtegemea kutokana na kwamba hakuna mtu anayeweza kuwapa kazi.
“Kula ni shinda, kunywa ni shida sina mtu wa kunisaidia. Ni mimi tu peke yangu,” Nespond alieleza.