Amuibia Polisi Simu ndani ya kituo cha polisi


Barobaro mmoja wa miaka 40 ambaye ni mkusanyaji takataka mwenye ujasiri amekiri mashtaka ya wizi wa kumuibia polisi


Akiwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Makadara Francis Kyambia, Joseph Kariuki alikiri shtaka la kuiba simu ya Konstebo Kibet Kirui ya KSh 19,500.


Mahakama iliarifiwa kuwa mnamo Jumapili, Aprili 16, Kirui aliacha simu yake ikiwa inachaji katika ofisi ya kupiga ripoti na kwenda kwa maankulii ya mchana na marafiki. Nation iliripoti kuwa aliporejea, Kirui hakupata simu yake, huku wenzake wakithibitisha kuwa hawakuichukua wala kuona na yeyote akiichukua.


Maafisa hao walikagua kamera katika kituo hicho, ambazo zilimnasa Kariuki akiiba simu hiyo afisini. Alihojiwa na polisi, ambao walimwonyesha picha hizo, lakini alisisitiza kwamba hakuiba simu. Hata hivyo, wakati wa kesi mahakamani, Kariuki alipiga abautani na kukiri kuiba simu hiyo. Aliomba mahakama imsamehe huku akirushwa rumande hadi Jumanne, Mei 30, akisubiri kuhukumiwa. Kwingineko, kanda ya CCTV inayoonyesha tukio ambapo mwizi aliiba simu ya mwanamke kwa njia ya ubunifu akiwa katika klabu jijini Nairobi imesambazwa kama moto kwenye mitandao ya kijamii.


Mwanamume huyo alionyeshwa akijifanya kupiga simu huku mrembo huyo akiwa amezama katika mazungumzo ya mapenzi. Katika video hiyo, mwanamume huyo alisubiri hadi mwanamke huyo na mpenziwe walipoanza kukumbatiana kisha kwa ustadi aliweka mkono wake juu ya meza na kuchomoa simu. Kisha alionyeshwa akiondoka haraka katika klabu ya OJ Lounge baada ya kuiba simu.


Jambo la kustajabisha ni kwamba mwanamume aliyekuwa akimrushia maneno matamu mrembo huyo naye pia aliondoka kwenye klabu hiyo baada ya wizi huo kufanyika.


Inasemekana kwamba wawili hao na mwanamume mwingine waliokuwa wameketi karibu na mwanamke huyo walikuwa katika genge moja. 

Chanzo:tovuti ya tuko


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo