SHAMSA FORD ATANGAZA TENA NDOA

Na Denis Mtima
KWA mara nyingine, mwigizaji wa filamu za nyumbani, Shamsa Ford ametangaza kufunga ndoa na mchumba’ke, Dickson Matoke aliyezaa naye mtoto na baadaye kuhitilafiana.
 
Shamsa Ford.

Katika mahojiano, Shamsa alifunguka kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kukaa chini na kutafakari juu ya maisha ya kukaa peke yake bila mwenzi wake huku baba wa mtoto wake akionesha upendo wa dhati kwake na mwanaye.

“Nimeamua kufanya hivyo kutokana na namna baba wa mwanangu anavyoonesha upendo kwangu na hata kwa mtoto wetu (Terry), kwa kweli namshukuru Mungu nitakapomaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na muda si mrefu vikao vya harusi vinaanza,’’ alisema Shamsa.

Alipoulizwa kuwa endapo akiolewa ataacha uigizaji, Shamsa alifunguka: Mchumba’ngu ni mwelewa hana kizuizi katika kazi yangu ya sanaa. Cha msingi ni kutimiza wajibu wangu wa kifamilia.”

Shamsa amekuwa akitangaza mara kwa mara kuwa atafunga ndoa na Dick baada ya kuishi naye kwa muda mrefu lakini matangazo hayo huwa hayazai matunda


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo