Imebainishwa
kuwa ni asilimia kubwa ya watoto wa kike hawamalizi shule kutokana
na kupewa mimba,kudanganywa na vitu vya thamani mbalimbali nakusababisa
kutofikia malengo yao ya maisha.
Hayo
yamebainishwa na muuguzi mkuu wa hospitali ya Mkoa wa manyara
Theonestina Rwechungura wakati alipokuwa akiongea kwenye mjadala
ulioandaliwa na mradi wa Je Nifanyeje? Unaofadhiriwa na
watu wa USAID mjadala huo ulifanyika katika chuo cha ufundi cha St
Joseph
kilichopo maeneo ya Dareda Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani wa
Manyara.
Alibainisha
kuwa siku hizi si kama miaka ya nyuma kwa mtoto wa kike kumaliza shule
au chuo
kutokana na kuwa na tama,kudanganywa na vitu nakusababisha kukatishwa
kwa
masomo pamoja na kupata ujauzito.
Alisema
kuwa mtoto wa kike anatakiwa kupatiwa elimu ya kutosha ili hapo baadaye
aeweze
kupambana na umaskini nasi kuwa tegemezi katika familia pamoja na jamii
kwa
ujumla.
Aliongeza
kuwa ukimwi umekuwa wimbi kila sehemu wanazungumzia
ukiwa shueleni,chuoni ili kuweza kutimiza malengo yao lazima
wajiheshimu,kujitunza,kujiamini pamoja na kujithamini.
Aidha
alisema kuwa ukiwa na tamaa utafanya vitendo viovu visivyofaa kwani
tafiti za
watoto wa kike wanakatishwa masomo kutokana na ujauzito hivyo wanatakiwa
wajilinde ili kuweza kutimiza malengo yao.
Alisema
kuwa wasichana
wanatakiwa wajifunze kusema hapana na wajifunze kukataa bali waendelee
na
masomo yao wajieupushe na mambo ya vishawishi ndio chanzo cha
vishawishi.
Kwa
upande wake mratibu wa mradi huo kutoka ‘Je Nifanyeje Diana
Nsindagi aliongeza kuwa mradi huo unalenga vijana hasa wa kike ili
kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiafya na kijamii amewataka watoto
wa
kike wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za baadaye.
Pia
alitaja mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kufanya maamuzi sahihi ya
kiafya na kijamii ni jiamini,jithamini,jitambue,jiheshimu,jiwekee
malengo,tambua mila na desturi zinazokuzunguka,tambua jamii
inayokuzunguka na
imani yao.
Wakichangia
mjadala huo washiriki hao ambao ni vijana wakike
wamesema kuwa watoto wa kike wanatakiwa wawe na msimamo na maamuzi
sahihi
ili baadaye weweze kusonga mbele,wawe na mpenzi mmoja,wamshawishi mpenzi
kupima
afya,kutumia kondomu pia waepuke na makundi mbalimbali.