Mustafa Kambona ambaye ni Msemaji wa Familia ya marehemu Benard Membe ametangaza ratiba ya mazishi ya kiongozi huyo mstaafu
Kambona amesema mwili wa marehemu utaangwa Jumapili Mei 14, 2023 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam
Amesema baada ya kuuaga mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kijijini kwao mkoani Lindi kwa Maziko yanayotarajiwa kufanyika Jumanne Mei 16, 2023

