SERIKALI YA KENYA YATISHIA KUWAFUKUZA KAZI WAALIMU WALIOPO KWENYE MGOMO


Mgomo wa walimu nchini Kenya

Serikali ya Kenya imetishia kuwafuta kazi walimu ambao wamekuwa wakigoma kwa wiki tatu sasa na kuwaajiri walimu wapya waliofuzu pamoja na walimu waliostaafu ikiwa hawatarejea kazini hii leo.

Makataa hii inakuja baada ya vyama vya walimu kukataa pendekezo la nyongeza ya mishahara ambayo wangelipwa kwa awamu tatu.

Walimu hao wanataka nyongeza ya aslimia miatatu ya mishahara, pesa ambazo serikali inasema haiwezi kumudu kwa sasa kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi. 

Mgomo wa walimu umesababisha kufungwa kwa shule za umma kwa zaidi ya wiki tatu sasa wakati wanafunzi wakijiandaa kwa mitihani ya kitaifa.

Huenda serikali ikalazimika kuakhirisha mitihani hiyo ya kidato cha nne na darasa la nane inayotarajiwa kuanza katika muda wa wiki chache zijazo.

Madaktari wa hospitali za umma pia wanafanya mgomo wa kitaifa huku hospitali hizo zikiwahudumia tu wagonjwa walio katika hali ya dharura.

SOURCE:BBC SWAHILI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo