"Akili Pia Ipimwe": Mahakama Yaamuru Yesu wa Tongaren Kuzuiliwa


Mahakama ya Bungoma iliyopo nchini Kenya imeagiza Eliud Wekesa maarufu kama Yesu wa Tongaren kuendelea kuzuiliwa ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi wao.


Katika uamuzi wake, Hakimu Mkuu Tom Olando aliwaruhusu polisi kumzuilia kwa siku nne mhubiri huyo ambaye hujidai kuwa Yesu.


Hakimu Olando pia aliwapa maafisa wa polisi ruhusa ya kumfanyie vipimo vya akili mshukiwa na kufanya msako katika boma lake la Tongaren.


Hili ni kufuatia oparesheni kali inayoendeshwa nchini dhidi ya wachungaji feki ambayo wanahubiri injili ya kupotosha na kuchochea itikadi kali miongoni mwa waumini wao. Yesu Wa Tongaren alijiwasilisha katika Kituo cha Polisi cha Bungoma kwa siku ya pili mfululizo kama alivyoagizwa na polisi lakini tofauti na Jumatano - akamatwa.


Wekesa alikamatwa asuhubi ya Alhamisi - 11 Mei 2023 na kufikishwa mahakama ya Bungoma lakini haijulikani ni kosa gani atashtakiwa kwalo. "Ndiyo, ni kweli yupo mahakamani hapa. Bado anasubiri hatua zijazo," mwandishi wa habari wa eneo hilo aliyeripoti tukio hilo aliiambia TUKO.co.ke. Jumanne, tarehe 9 Mei, polisi katika kaunti ya Bungoma walimuita Yesu Wa Tongaren kuhusiana na madai ya shughuli za kikundi cha kidini katika kanisa lake.

Chanzo:tuko.co.ke



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo