ASILIMIA 28 YA WAKAZI WA DODOMA HAWANA VYOO

ASILIMIA 72 ya wananchi wa mkoani Dodoma hawana vyoo bora huku asilimia 28 wakijisaidia katika vichaka na maeneo ya wazi.

Haki hiyo inaelezwa kusababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira na kuhatarisha usalama wa afya za wananchi katika wilaya zote mkoani hapa.

Ofisa Afya Mkoa wa Dodoma, Edward Ganja, amebainisha hayo mjini hapa katika mafunzo kwa waandishi wa habari yaliondaliwa na Shirika la Plan Internatinal.

Amesema utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mapema mwaka huu mkoani Dodoma unaonyesha idadi kubwa ya wananchi hususan vijijini wamejenga vyoo visivyo na ubora ambavyo ni hatari kwa usalama wa afya.

“Ukiona mabanda ya vyoo ni yale yaliyojengwa kwa makuti bila kupauliwa ambayo hujulikana kama ‘pasipotisaizi’ ambapo hakuna faragha kwa kuwa mtu akiingia sehemu ya kichwa huonekana wazi,” amesema Ganja.

Ameeleza kuwa wilaya za Kongwa, Chamwino na Bahi zinaongoza kwa vifo vingi vya watoto walio chini ya miaka mitano kutokana na kukosa vyoo bora na kusababisha vinyesi kutapakaa sehemu za wazi, mashambani, kwenye vyanzo vya maji na kwenye makazi ya watu na kusababisha milipuko ya magonjwa.

“Kweli juhudi kubwa zinahitajika kuwahimiza wananchi kwani utafiti unabainisha asilimia 27 tu za kaya zenye vyoo bora katika mkoa wa Dodoma, hii ni hatari sana,” amesema Ganja.

Aidha, aliwataka wananchi kutunza mazingira kwa kujenga vyoo bora na kuachana na tabia ya kujisaidia sehemu za wazi.

Kwa mujibu wa Shirika la Plan Internatinal Watanzania watoto 36,500 wakiwemo watoto 18,500 wanapoteza maisha kutokana na kuharisha na asilimia 90 kuugua kutokana na maji machafu, mazingira machafu na kushindwa kunawa vizuri kabla na baada ya kutoka chooni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo