Walimu 13 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamefukuzwa kazi kutokana na makosa ya utoro huku wengine wanne wakiendelea kujadiliwa kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo kujihusisha na mapenzi na wanafunzi pamoja na ulevi uliopindukia katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2020 hadi Septemba mwaka huu
Katibu wa tume ya utumishi wilayani humo Fedinand Ndomba amesema tabia ya utoro inayofanywa na baadhi ya walimu imekua ikichangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu.