MWENYEKITI WA UVCCM SINGIDA ASIMAMISHWA KAZI

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida limemsimamisha uongozi Mwenyekiti wao wa mkoa, Martin Labia Lissu kwa madai ya kushindwa kutoa utetezi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Katika kikao chake kilichofanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Singida na kuhudhuriwa na wajumbe 24 wa baraza hilo kwa kauli moja wameridhia hatua hiyo na kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Joseph Saenda aliwaambia waandishi wa habari kuwa kikao kilikuwa na agenda moja ya kumwita mbele ya baraza mwenyekiti wao, Lissu.

Alisema baraza baada ya kujadiliana kwa pamoja, wajumbe hawakuridhishwa na majibu ya utetezi wake, kwani hakuonesha kukiri kufanya makosa mbele ya wajumbe wa kikao.

“Baada ya mjadala wa muda mrefu baraza limemsimamisha uongozi, kwa mujibu ya katiba ya UVCCM ibara ya 78 (i) na kutoa mapendekezo ya kumvua uongozi kwa ngazi ya juu yenye mamlaka hayo kikatiba,” alisistiza.

Mei 17 mwaka huu, wajumbe wa baraza hilo kwa kauli moja walidai kutokuwa na imani na uongozi wa mwenyekiti huyo kutokana na kutumia vibaya madaraka yake na kuwa mtovu wa nidhamu na kudharau viongozi wa juu wa chama.

Saenda aliorodhesha tuhuma zilizokuwa zikimkabili Mwenyekiti huyo kuwa ni kushindwa kuitisha vikao tangu achaguliwe mwaka 2012 na kushindwa kushiriki ziara mbalimbali za viongozi ndani ya chama. 

Mwenyekiti huyo pia alikuwa akituhumiwa kuwa mchonganishi kati ya viongozi wa UVCCM na chama na kushindwa kufanya kazi zake na badala yake kujikita zaidi kwenye kampeni za mmoja wa wagombea nafasi ya urais mwakani. 

Meneja wa duka jipya la huduma kwa wateja la Vodacom lililopo Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam, Swaum Manengelo akifungua mlango kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo uliofanyika juzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo