Ujenzi wa barabara ya muungano inayounganisha vijiji vitatu ambavyo ni Imehe, Ugabwa na Ilevelo umepokelewa kwa shangwe na wananchi wa vijiji hivyo ambayo imetengenezwa kwa kutumia michango ya wananchi na wadau wa vijiji hivyo waishio nje
Wananchi wa vijiji hivyo vitatu wamekutana Oktoba 20, 2022 katika eneo la Ngwamanga kujadili suala la maendeleo ya barabara hiyo ambayo tayari imetoka kijiji cha Imehe hadi Ilevelo na kwa sasa inafuata ya kuelekea kijiji cha Ugabwa
Barabara hiyo imezungumzwa kwa muda
mrefu namna itakavyoweza kujengwa ili irahisishe mawasiliano, hivyo kwa kupitia
wananchi wa vijiji hivyo na wazawa wa vijiji hivyo wanaoishi nje wameweza
kufanikisha hilo, kama anavyoeleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilevelo Seso
Mahenge aliyesisitiza pia kwamba manufaa ya barabara hiyo yataanza kuonekana siku chache zijazo
Mwenyekiti wa Kamati ya Muungano wa Barabara hiyo Daudi Kyando amesema wanakusudia kufufua soko walilokuwa wanalifanya wazee wao kipindi cha nyuma huku Katibu wake Alfa Mahenge akizungumzia suala la kuanzishwa Jumuia itakayoleta umoja wa vijiji hivyo
Mwenyekiti wa Kijiji cha Imehe Audensi Mahenge amesema mojawapo ya kikwazo walichokumbana nacho ni pamoja na kuwepo kwa jiwe kubwa lililowalazimu kutumia baruti kulipasua ili barabara hiyo iweze kujengwa
Soja Mahenge, Edson Sanga, Mwl. Frank Sanga, Huruma Kyando, Jane Sanga na Erestina Kyando Ni miongoni mwa wananchi waliohudhuria mkutano huo kila mmoja akizungumzia ujenzi wa barabara hiyo na manufaa yatakayopatikana huku wengi wao wakiona manufaa yaliyopo katika kilimo, kwani itawarahisishia katika shughuli za kilimo kwa kufika mashambani na kusafirisha mazao yao kirahisi