Serikali imetenga zaidi ya bilioni 270 kwa ajili ya miradi ya Maji
vijijini kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 chini ya mpango wa utekelezaji
matokeo makubwa sasa ambapo vijiji 1,239 vitanufaika na huduma hiyo.
Hayo yamesemwa bungeni na waziri wa Maji Mh Prof Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha bajeti yake ya makadirio na matumizi kwa mwaka 2014/2015.
Aliainisha kuwa kazi zitakazotekelezwa ni ujenzi na upanuzi wa miradi ya Maji pamoja na ukarabati wa miundo mbinu ya Maji.

Kukamilika kwa miradi hiyo itakuwa na ongezeko la vituo 28,031 vya kuchotea Maji vitakavyohudumia jumla ya wakazi milioni 7 wanaoishi vijijini.
Prof Maghembe aliainisha kuwa kwa mwaka wa fedha unaoisha 2013/2014 kiasi cha Bilioni 236 ilikasimiwa kwa ajili ya kutekeleza mirdi ya Maji vijijini ambapo serikali imezipatia Halmashauri na Sekretariati za mikoa zaidi ya bilioni 137 kwa ajili ya utekelezaji na usimamizi wa mradi wa Maji wa vijiji 10 kwa kila halmashauri.
Aidha kwa mwaka wa fedha uliopita zaidi ya bilioni 10 zimeelekezwa kwenye miradi mingine ya Maji vijijini kama vile miradi yenye kuleta matokeo makubwa sasa, ujenzi wa Mabwawa, mradi wa Same-Mwanga-Korongwe na gharama za ziada za usimamizi na ufuatiliaji wa miradi.