Daktari wa Membe afunguka kuhusu kunyweshwa sumu

Daktari wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Bernard Membe, ameondoa sintofahamu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe na kusema hajauawa bali kifo chake kimetokana na maambukizi ya ghafla ya mapafu yaliyopelekea damu kuganda.


Profesa Haruni Egoli, ambaye ni Daktari mwandamizi na msahuri wa maradhi ya ndani na maradhi ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Muhimbili, ni daktari wa familia na daktari binafsi wa Membe.

"Kwa kifupi niseme, Mh. Membe amekuwa mzima kwa miaka mingi, hajawahi kuwa na tatizo lolote la magonjwa sugu kama ya Sukari, Presha, Magonjwa ya moyo hajawahi kuwa nayo.

"Kilichotokea ni kwamba amepata maambukizi ya ghafla ya mfumo wa mapafu hewa, ambayo imepelekea akapata mgando wa damu kuwa nzito na kusababisha mapafu kushindwa kupeleka oxygen (kitaalam inaitwa pulmonary embolism)".

"Hii inatokea mara kwa mara sana kwa mtu anayepata maradhi ya pneumonia ambayo husababisha damu kuganda.

"Kwa hiyo niondoe tafrani na mkanganyiko unaendelea huko mtaani kwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda Membe ameuawa au amenyweshwa sumu, au matatizo mengine hapana hiyo ni hali iliyopo, nalieleza Taifa, tatizo hili anaweza kupata mtu yeyote hata mimi".

"Membe amepumzika yuko katika mazingira hayo, hakuna kingine cha kusema nje ya sababu ya hiyo ya kifo," amesema Daktari huyo.

Taarifa za kifo cha Bernard Membe zimetoka leo Mei 12, na tayari viongozi mbalimbali wa Kiserikali wanaendelea kutoa salamu za Rambirambi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo