Mwalimu katika Kaunti ya Nyamira nchini Kenya amelazwa katika hospitali ya Ikonge baada ya kushambuliwa na mwalimu mkuu kwa madai ya kuchelewa kufika shuleni.
Mwalimu huyo wa Sekondari aitwaye Vincent Onyancha amesema alifanyiwa vurugu mbele ya wanafunzi wake darasani wakati akifundisha ambapo mkuu huyo alimpiga makofi na kumpiga mateke kisha kumburuza hadi ofisini kwake ambako aliendelea kumpiga.
Maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET) wamelaani tukio hilo na kuitaka Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu mkuu huyo. Hata hivyo TSC imesema imeanza kufanya uchunguzi.