Wafuasi Chadema wamzomea Ryoba, wamuita 'Yuda msaliti'


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Samuel Ghati amesema chama hicho kimepitia wakati mgumu baada ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo mbunge kuhamia Chama Cha Mapinduzi wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tano.

Ameyasema hayo mjini hapa jana Machi 15, 2023 alipokuwa akifungua mkutano wa hadhara ambao unatarajiwa kuhutubiwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine.

Hata hivyo, wafuasi wa chama hicho wamemzomea aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo alipokaribishwa kupanda jukwaani.

"Wilaya yetu awali ilikuwa ni ngome ya Chadema lakini baada ya viongozi wetu kuhama kwakweli tulipitia wakati mgumu sana lakini kwa mwitikio huu naamini 2025 jimbo litarejea kwetu," amesema.

Amewataja viongozi wengine waliohama pamoja na Mbunge Marwa Ryoba ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya, katibu wa wilaya pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo