KIJANA AUAWA KWA SILAHA ZA JADI NA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA NG'OMBE WA BABA YAKE MZAZI SHINYANGA

Matukio ya wananchi kuendelea kujichukulia sheria mkononi limeendelea kushika kasi mkoani Shinyanga ambapo huko katika kijiji na kata ya Busoka wilaya ya Kahama kijana mmoja ameuawa kikatili kwa kushambuliwa kwa silaha za jadi kisha kuchomwa moto baada ya kuiba ng’ombe wa baba yake mzazi.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea Aprili 8,mwaka huu saa tisa alasiri,ambapo wananchi waliojichukulia sheria mkononi kumshambulia kwa silaha za jadi kisha mwili wake kuuchoma moto.
 
Kamanda Mangalla amemtaja kijana huyo kuwa ni Shida Petro(17) mkazi wa Bugarama wilayani Kahama ambaye ameuawa kikatili kwa kushambuliwa kwa silaha za jadi kisha mwili wake kuchomwa baada ya kumtuhumu kuiba ng’ombe watatu wa baba yake mzazi aitwaye Petro Sangashelile ambao walimkuta nao na kuanza kumshambulia na kusababisha kifo chake

Tayari jeshi la polisi linawanawashikilia watu tisa kuhusiana na tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo