Mke wa Rais na Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,wama, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Jhpiego nchini Tanzania, Bi Maryjane Lacoste
kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki kulikofanyika sherehe ya kutimiza miaka
40 ya shirika hilo tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Maryrose Giattas, Cervical Cancer
Prevention Program Adviser wa Shirika la Jhpiego kwenye maonyesho ya huduma
mbalimbali zitolewazo na shirika hilo. Maonesho hayo yalifanyika katika hoteli
ya Doubletree ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 40 ya shirika
hilo.
Mama Salma Kikwete
akipata maelezo kutoka kwa Dr. Hokororo wa shirika la JHPiego juu ya kuhifadhi
vifaa vinavyotumika katika suala zima la afya ya mama na
mtoto.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka 40
ya shirika la Jhpiego huko Doubletree hotel Masaki. Kulia kwa Mama Salma ni Dr.
Leslie Mancuso, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego akifuatiwa na Bi Sharon Cromer,
Mkurugenzi wa Shirika la USAID nchini Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid akifuatiwa na Dr Allan Damiba, Jhpiego Senior
Vice President na wa mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema,
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.