BINTI WA MIAKA 25 ALIYEJIFUNGUA WATOTO WANNE MBEYA AZIDI KUPATA MISAADA

Na Saimeni Mgalula
Mkazi mmoja Aida Nakawala (25) wa kijiji cha Chiwanda,Wilaya ya Momba, mkoani mbeya ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya wazazi ya Meta,amepokea misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwaajili ya kituo cha kuleleA watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole jijini hapa.


Hata hivyo misaada hiyo imepitia katika Mtandao wa Kijamii wa Mbeya yetu ambapo msaada wa kwanza umepokelewa hivi karibuni wenyethamani ya shilingi Laki moja kutoka katika familia ya masawe wa Dar es Salaam kwa ajili ya kituo hicho ambapo mbeya yetu iliuwakilisha kama ulivyo..


Pia mbali na msaada huo mtandao huu huu ukishirikiana na Mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Dar es Salaam wa
www.issamchuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa msamaria mwema wa Uingereza,Bi Gladness Sariah ambaye alitoa mabiksi ya nguo na vitu kadhaa vya wa Watoto.

Kutokana na Watu kugushwa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne ambao wanaendelea Vizuri pia msamaria Mwema mwingine alijulikana kwa jina la Dada Norah SilverButtique toka DSM ambaye alitoa maziwa lactogen dazani mbili yani makopo 24 na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya mbeya yetu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo