Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wamekuwa ni mitazamo tofauti kutokana na kutokuwa na mabadiliko ya bei ya nauli za Makete Njombe kwani bei zilizokuwa zinatumika wakati barabara haijajengwa kwa kiwango cha lami ndizo zinazotumika na sasa ambapo barabara hiyo tayari imejengwa kwa kiwango cha lami
Katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Februari 24, 2023 madiwani hao wamesema ni wakati wa kulivalia njuga suala hilo kwa kuwa kiwango cha shilingi 10,000 wanachotozwa wananchi kama nauli tangu barabara hiyo ikiwa ya vumbi, ndicho kinaendelea kutozwa mpaka sasa ilivyojengwa kwa lami jambo wanalosema sio sawa.
Tazama Video Hii hapa Chini