Watu sita wakiwemo waganga wa kienyeji watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kuwapa dawa wahalifu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ili wasijulikane walipo watakapotafutwa na jeshi la polisi
Watu hao pia wanatuhumiwa kujihusisha na kupiga ramli chonganishi zinazosababisha mauaji na ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema waganga watatu wa kienyeji wamewakamata baada ya kupata taarifa za siri na kufanya uchunguzi kisha kufanikiwa kuwakamata wakiwa na baadhi ya vifaa wanavyotumia kufanya kazi ya kuosha dawa wahalifu ili wakitafutwa wasionekane walipojificha
Katika hatua nyingine Kamanda Magomi akazungumzia wizi wa dawa na vifaa tiba uliofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu katika zahanati ya Ilola Halmashauri ya Shinyanga na kuisababishia hasara serikali huku wakiwashikilia watu watatu akiwemo mlinzi kwa tuhuma za wizi wa dawa na vifaa tiba ambazo zimekutwa nyumbani kwa mtu.
Jeshi la polisi linaendelea kufanya kuchunguzi ili kubaini waganga wa kienyeji wanaopiga ramri chonganishi na kuwaosha dawa wahalifu.