Akutwa akiwa Hai kwenye Chumba cha Kuhifadhia Maiti


Msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye aliripotiwa kufariki baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali  kwa madai ya kuiba ndizi katika mji wa Apac, Uganda, amepatikana akiwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti, saa chache kabla ya uchunguzi  wa kifo chake kuanza.


Mwathiriwa huyo ambaye ni mkazi wa Kata ya Matimia katika tarafa ya Arocha, aliripotiwa kupatikana akiwa hai wakati madaktari katika Hospitali ya Apac wakijiandaa kufanya upasuaji baada ya kufariki dunia.

msemaji wa polisi wa mkoa wa Kyoga Kaskazini, Bw Patrick Jimmy Okema, amesema kuwa  "Taarifa zilipokelewa kwamba alifariki  baada ya kupigwa na kundi la watu wakimtuhumu kwa wizi. Maafisa wetu walizuru eneo la tukio, walirekodi taarifa na kuufikisha mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya Apac,"

Hata hivyo, wakati madaktari hao wakijiandaa kufanya postmortem, waligundua kuwa bado yuko hai, akapelekwa  wodini kwenye mashine ya kusaidia maisha na bado yupo kwenye uangalizi maalum.

Mtu mmoja anashikiliwa kutokana na tukio hilo. Aliwaonya walioko mbioni kujisalimisha polisi kabla ya kutafutwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo