Diwani aliyepotea tena, mke akiri kuchoka, adai hamtafuti tena

Mke wa Diwani wa Kawe, Mutta Rwakatare, amekiri kutokujua ni wapi alipo mume wake huyo kwani hadi sasa unakaribia mwezi wa tatu bila diwani huyo kuonekana nyumbani na kusema amechoka na tabia hizo na hatohangaika tena kumtafuta.


Hayo ameyabainisha hii leo Novemba 17, 2022, wakati akizungumza na vituo vya habari vya East Africa TV & Radio digital, mke wa Mutta amesema kuwa awali alipopotea alikutwa kwenye moja ya gesti zilizopo wilayani Kinondoni akiwa na mwanamke na walifanikiwa kumrudisha nyumbani lakini baadaye alitoweka tena hadi leo.


Ikumbukwe awali diwani huyo alipotea ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilieleza kumpata akiwa nyumbani kwa Ashura maeneo ya Tabata Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo