Studio ya Bob Junior imebadilika kutoka ‘Sharobaro Records’ na kuwa ‘Sharobaro Music’.
Bob Junior ameiambia Kikwetu Blog kuwa sababu za kubadilisha jina
hilo ni kutokana na kubadilika kwa muziki atakaokuwa akiutengeneza kama
mtayarishaji wa muziki na pia kutokana na kununua vifaa vipya.
“Ilikuwa ni mahesabu ya kwangu mimi na kampuni yangu, tulikuwa
tunataka kuibadilisha kuanzia muziki, sound kwasababu kuna vyombo vipya
ambavyo vimekuja kutoka Marekani na pia nilikuwa nimetengeneza sound
mpya siku nyingi,” amesema.
Mtayarishaji huyo wa muziki amedai kuwa uamuzi huo umekuja ili
kuwathibitishia watu kuwa anaweza kufanya muziki wa aina mbalimbali.
