Polisi na Raia watandikana Makonde ndani ya kituo cha Polisi

Kisanga kimeshuhudiwa katika kituo cha Polisi cha Kati mjini Nakuru Kenya baada ya polisi na raia kukabana koo.


Kwenye video ambayo inasambaa mtandaoni, wawili hao wanaonekana wakirushiana makonde mazito ndani ya eneo la kurekodi matukio.


Afisa aliye na sare rasmi za kazi anaonekana akimwendea raia huyo na kuzungumza naye kabla ya kumlima kofi moja safi. Ni jambo linalomkera jamaa huyo na ghafla bin vuu anamrushia afisa huyo konde moja nzito na kufanya ateguke.


Maafisa wengine wa polisi pamoja na raia wanakimbia kuokoa hali na kuhakikisha kuwa wawili hao wanaacha kulimana. Kwa mujibu wa jamaa mmoja aliyeshuhudia kisa hicho, mzozo ulizuka wakati wa kurekdoi kisa cha uhalifu. "Jamaa huyo alikuwa amefika hapo kurekodi kisa lakini mzozo ukatokea," aliyeshuhudia alisema. 

Duru katika kituo hicho zinaarifu kuwa OCPD ametakiwa kutoa taarifa kwa wakubwa wake kuhusiana na kisa hicho.


Katika kaunti ya Homa Bay, afisa mmoja anayesimamia kituo cha polisi yuko pabaya baada ya majambazi kuvamia kituo chake na kuhepa na bunduki nne. Bado haijabainika ni vipi kisa hicho kilifanyika ndani ya kituo cha polisi ambapo kwa kawaida usalama huwa ni mkali. Polisi katika kituo hicho kilicho eneo bunge la Mbita walisema wezi hao walivamia eneo ambapo silaha huwekwa. 


Waligundua baadaye kuwa bunduki nne pamoja na ngunia la risasi 110 zilikuwa zimetoweka na hivyo kuanza msako. Mkuu wa polisi katika eneo la Homa Bay Samson Kinne amedhibitisha kisa hicho huku akisema uchunguzi unaendeshwa kuhakikisha wahusika wamekamatwa.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo