Polisi yatoa amri kukamatwa wabunge wa CHADEMA

Jeshi la Polisi Nchini leo Machi 22, 2018 limetoa amri ya kukamatwa kwa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa jimbo la Tarime, Esther Matiko kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuitikia wito wa jeshi la polisi

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa jeshi la polisi limeagiza wabunge hao wakamatwe popote walipo na kufikishwa kituoni kutokana na kushindwa kufika katika wito huo leo.
Aidha viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Mashinji na Salum Mwalim ambao walifika polisi kuitika wito huo mapema leo waliachiwa majira ya mchana wakiwa hawajahojiwa kitu chochote na kuambiwa warudi tena Jumanne 27, 2018.
Mbali na hilo jeshi la polisi liliendelea kuwashikilia Mbunge John Mnyika na John Heche ambao walibaki kituoni hapo na kufanyiwa mahojiano na kisha baadae kuruhusiwa kuondoka


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo