Jeshi la Polisi Mkoani Songwe linawashikilia watu 3 wa familia moja wote wakazi wa kijiji cha Ihowa wilayani Mbozi akiwemo Baba Mzazi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanafamilia Bi. Anna Julius Mwasimba(30) wakati akifanyiwa maombi baada ya kusumbuliwa na maradhi kipindi kirefu ambapo alirudi kutoka Mbeya alikokuwa akiishi ili kupatiwa huduma za maombezi.
Kamanda wa Polisi Songwe ACP Alex Mkama amesema mnamo tarehe 15 Novemba Mwaka huu tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho ambapo mpaka sasa baba pamoja na watoto wake 2 wanashikiliwa kwa ajili ya tukio hilo.
Baadhi ya ndugu na majirani katika kijiji hicho wamesema tukio hilo limewasikitisha.
