Mtoto aliyejirekodi kuhusu kubadilishiwa namba apongezwa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amempongeza mwanafunzi Iptisam Suleiman Slim mtahiniwa wa kituo cha mtihani cha shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic kwa kutambua na kupigania haki yake ambapo alirekodi video clip akieleza kuwa alibadilishiwa namba ya mtihani wakati akifanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) uliofanyika tarehe 05 na 06/10/2022.


Baada ya kufanyika Uchunguzi imebainika kuwa katika shule hiyo jumla ya watahiniwa saba walibadilishiwa namba za mtihani na Serikali imeifungia shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic kuwa kituo cha mitihani kwa muda usiojulikana na Pia Waziri Mkenda ameagiza walimu wote waliohusika wasimamishwe kazi.

Waziri Mkenda amesisitiza kuwa shule yoyote itakayobainika kufanya vitendo vya udanganyifu wa mitihani, itafungiwa na hata kufutwa kabisa kuendesha shughuli za elimu nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo