Magufuli Akataa Kutumia Helikopta.......Asema Atatumia Gari ili Azijue Kero za Wananchi

Pazia la kampeni za uchaguzi mkuu limefunguliwa rasmi mikoani kwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli kuwahutubia wakazi wa mkoa wa Katavi huku akiwaahidi wananchi kuiunganisha kwa barabara za lami mikoa ya Rukwa na Katavi ili wananchi waweze kuinua uchumi wao kwa kusafirisha mazao.

Ikiwa ni uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mikoani baada ya tume ya taifa ya uchaguzi kupuliza kipyenga chake jumapili ya August 23 ya mwaka huu mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr John Pombe Magufuli amehutubia mikutano mitatu katika maeneo ya makazi ya waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa 1972 ya mishamo kilimomita zaidi 150 kutoka mjini Mpanda, kisha makazi ya katumba na baada katika mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mpanda na kuahidi kuwatatulia kero ya kosefu wa barabara inayosababisha kushindwa kupeleka mazao yao sokoni kutoka katika mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa kwa kuiunganisha na mikoa mingine ya Tanzania.
Katika maeneo ya makazi ya waliokuwa wakimbizi kutoka Burundi wa 1972 ambao kwa sasa ni raia halali wa Tanzania mara baada ya kupewa hadhi hiyo na serikali Dr Magufuli amewondoa hofu na kuwataka kuishi kwa amani na upendo kama walivyo watanzania wengine huku akiwahidi kuwapelekea huduma za msingi za binaadamu ikiwemo maji, umeme, barabara na hospitali.
Waziri mkuu Mh Mizengo Kayanza Peter Pinda ndie aliyekuwa mwenyeji wa mgombea huyo wa kiti cha urais kupitia CCM huku akimtambulisha kama jembe linaloweza kuipaisha Tanzania kwa maendeleo ya haraka kwa kuwa anachukia uzembe, ubadhirifu rushwa na ufisadi na kwamba chama hicho hakikufanya makosa kumchagua.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo mkubwa wa hadhara katika uwanja wa kashaulili mjini Mpanda wamesema kiongozi ajaye lazima awe na ujasiri wa kupambana na vitendo vya rushwa hususani katika ofisi zilizopo chini ya serikali za mitaa pia mafisadi papa kwani wamechangia kwa kiasi kikubwa watanzania wengi kuishi katika umasikini uliotokea huku wao wakiishi maisha ya peponi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo