LINDI
Watu 60 wamekufa mkoani Lindi katika ajali 193 za barabarani zilizotokea kati ya Januari na Desemba mwaka jana huku wengine 310 wakijeruhiwa ambapo baadhi yao wamepata ulemavu wa kudumu
Hayo yamebainishwa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Lindi George Mwakajinga ambapo amebainisha kuwa idadi hiyo ya vifo imepungua ikilinganishwa na vifo 72 vilivyotokea mwaka 2010 katika ajali 172 zilizosababisha majeruhi 275
Amesema kati ya ajali hizo 48 wahusika wamefikishwa mahakamani ambapo wamepatikana na hatia na kupewa adhabu mbalimbali 35 bado zipo mahakamani 28 zimefutwa na zilizosalia 82 bado uchunguzi unaendelea