Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mh. Jesca Msambatavangu ameelezea tatizo la wivu wa kiongozi wa sehemu ya kazi kupinga mafanikio ya mfanyakazi anayemwongoza kuwa ni mojawapo ya viashiria vya tatizo la Afya ya Akili.
Mh. Jesca Msambatavangu amesema kiongozi asiye na maarifa ya kutosha huona wivu kwa wafanyakazi anaowaongoza badala ya kuwatumia kufikia malengo aliyowekewa.