Polisi katika kaunti ya Kisumu nchini Kenya wameanza uchunguzi wa mauaji ya msichana wa miaka 18 ambaye mwili wake ulipatikana katika shamba la mpunga.
Kituo cha Citizen TV kimesema kulingana na familia, msichana huyo Wendy Abura aliondoka nyumbani kwao Jumatatu usiku ili kupokea simu, lakini hakurejea.