Tumeridhishwa na Utekelezaji wa Miradi - Kamati

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo.


Hayo yamesemwa Oktoba 19, 2022 na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mhe. Mecksedeck Kabelege wakati wa Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka.

Mhe. Kaberege amesema kuwa pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili miradi hiyo ikiwemo Jiografia za maeneo hayo bado miradi hiyo imetekelezwa kwa kiwango na ubora mkubwa.

"Pamoja na mapungufu kwenye maeneo machache bado miradi hii inaonekana kujengwa kwa kiwango kikubwa na thamani ya fedha inaonekana"

Kwa upande wake Mhe. Rhoida Wanderage Diwani wa kata ya Mtwango wa amewataka viongozi ambao wanaenda kutekeleza miradi mbali mbali kwa kipindi hiki waende wakajifunze kwenye maeneo mengine ambayo tayari wameshatekeleza miradi kama hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Agustino Nyenza amesema kuwa wataalam na uongozi wataendelea kushirikiana na wananchi katika suala la uibuaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Tayari Mkurugenzi wetu Mtendaji Sharifa Yusuf Nabalang'anya ameanza kushiriki na wananchi kwenye ujenzi wa madarasa ya sekondari kupitia fedha zilizotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuanzia hatua ya Msingi ili kuhakikisha katika kila hatua ya ujenzi huo unafanyika kwa kiwango na ubora unaotakiwa" Alisema Nyenza.

Miradi iliyotembelewa leo ni Ujenzi wa Zahanati ya Welela kata ya Mtwango, na Zahanati ya Lole kata ya Ikuna, Ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari Ikuna kata ya Ikuna na Utekelezaji wa Mradi wa Maji Shule ya Sekondari Kidegembye kata ya Kidegembye.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo