MCHUNGAJI wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar es Salaam, Eliona Kimaro, amesema kauli
za ‘vyuma vimekaza’ na ‘pambana na hali yako’ ni za kuzimu na hazipaswi kuendelea kuwepo mwaka huu.
Akihubiri wakati wa ibada ya mkesha wa Mwaka Mpya usiku wa kuamkia Januari 1 mwaka huu, Kimaro alisema kauli hizo zilitawala mwaka jana na si vema watu
wakavuka nazo.
“Mapepo ya mateso yanakuja mahali hadi yanatengeneza mapambio na watu wanasema usihangaike na mimi pambana na hali yako… ni sentensi za
kuzimu.
“Hizi sentensi hazitavuka 2018, nazifuta kwa damu ya Yesu,” alisema