Serikali ya Tanzania imewataka waombaji wa kazi kuzingatia taratibu zinazotakiwa katika kuwasilisha maombi ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kuwepo wa tatizo la kuwasilisha nyaraka pungufu.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi
wa Umma, Riziki Abraham amesema kumekuwepo na kutokufuata taratibu kwa
waombaji wa kazi kutoka na baadhi yao kuwa na nyaraka ambazo hazikidhi
vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa tangazo la kazi.
Hata hivyo Bi. Riziki amewataka wote ambao wamepotelewa, kuharibikiwa na vyeti vya kitaaluma wanatakiwa kupeleka taarifa za kupotelewa katika mamlaka husika ili waweze kupewa taratibu za kupata vyeti vingine.
Wakati huo huo, Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi Nchini (Veta) Nyanda za Juu Kusini, imefunga vyuo saba vya binafsi vya mafunzo ya hoteli na utalii Nyanda za Juu Kusini kutokana na kukiuka taratibu kwa kuendesha mafunzo bila kusajiliwa.
Mratibu wa Veta Nyanda za Juu Kusini, John Mwanja, amesema kuwa wamefikia hatua ya kuvifunga vyuo hivyo kutokana na kukosa sifa za kutoa mafunzo kutokana na kutokidhi vigezo ikiwemo usajili na vifaa vya kujifunzia.
Miongoni mwa vyuo vilivyofungwa ni Msoma Utalii tawi la Njombe, Eckross Tourism Collage,Chuo Cha Utalii Mosemi na Hokaido VTC kwa mkoa wa Njombe,na Capricon Collage, Iringa Hotel and Tourism Collage na Mufindi Tourism Collage vyote vya Mkoa wa Iringa.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo hivyo walilalamikia hatua ya wamiliki wa vyuo hivyo kwa kuwadanganya kuwa vyuo hivyo vimesajiliwa ilihali havijasajiliwa na hivyo kuwaibia wananchi na kuiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Katika hatua nyingine, nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo SADC zimetakiwa kuondolewa kanuni na vikwazo vinavyokwamisha biashara na kurudisha nyuma jitihada za wanachama kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara kutoka wizara ya viwanda na biashara Ismail Mfinanga katika mkutano wa wanachama wa jumuiya hiyo amesema vikwazo katika baishara ndani ya nchi wanachama vimekua vikitokea kutokana na mawasiliano duni.
Mfinanga ameongeza kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutaweza kukuza masoko ya wanachama pamoja na kuongeza uhuru wa masoko ya bidhaa kwa jumiya hiyo katika masoko ya nje.
Mkutano huo unasharikisha Wizara mbalimbali ikwemo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Chakula na Kilimo pamoja na shirika la viwango Tanzania (TBS)