Mchora katuni maarufu ya SOKOMOKO Thaddei Thomas Marealle, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Kairuki, taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa kaka ake William G Marealle Mikocheni jijini Dar es Salaam
Marehemu alijipatia umaarufu kupitia Katuni za Sokomoko zilizokuwa zikichapishwa kupitia gazeti la Sani lililojipatia umaarufu sana miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000
Kupitia gazeti hilo zilikuwepo katuni nyingine maarufu kama vile Kifimbo, Kipepe, Harakati a Pimbi, Ndumila kuwili, Lodi lofa, Madenge, Sukununu za babu Sani, Bush Star na Born Town.