Basi la kampuni ya Mwafrika linalofanya safari zake Iringa-Makete likishusha abiria stendi mpya ya Tandala
Wananchi waliohudhuria kikao cha maboresho ya stendi hiyo mpya
Mkuu wa wilaya ya Makete mh Daud Yassin akizungumza kwenye kikao hicho
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo akifafanua jambo kwenye kikao hicho
Mkazi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete Yusuf Kisimbilo akichangia hoja ambapo alisisitiza serikali kuboresha mifereji ya maji katika stendi hiyo
Mama ntilie, Tabia Ilomo akizungumzia namna barabara ya kutokea kwenye stendi hiyo ilivyowekwa eneo la hatari
Wananchi wakiendelea kutoa maoni yao
Mtaalamu kutoka ofisi ya mhandisi wa ujenzi wilaya ya Makete Jumanne Majenzi akijibu hoja za wananchi katika kikao
Basi likiingia kwenye stendi hiyo mpya
Afisa biashara wa wilaya Edonia Mahenge akiendelea kujibu hoja zinazomuhusu katika kikao hicho
Vibanda vya wafanya biashara vilivyopo kwenye stendi mpya ya Tandala
Eneo la kutokea linalolalamikiwa kuwa na mteremko mkali
Mkuu wa wilaya ya Makete Daudi Yassin (kushoto) akiwa na diwani mteule wa kata ya Tandala Egnatio Mtawa
Kikao cha kupokea maoni ushauri na maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya Tandala kimefanyika jana katika stendi hiyo
Kikao hicho kimewakutanisha wananchi na viongozi wa wilaya ya Makete ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuboresha changamoto ndogondogo zilizojitokeza ili stendi hiyo ianze kutumika rasmi