Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu amedai kuwa kuna dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali.
Lissu, amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi huku akionekana kuilaumu serikali kwa kuwakandamiza wapinzani.
Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa Jumuia ya kimataifa kuingilia kati akisema kwa madai kuwa hali nchini Tanzania imebadilika.
Amesema,hadi sasa anaamini kuwa hakuna uchunguzi wowote unaofanywa kuhusu kushambuliwa kwake Septemba 7, mwaka jana.
Tazama video Hii hapa chini:-