Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017Leo asubuhi baada ya Ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma. pic.twitter.com/73crlwVZpu— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) December 17, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli tarehe 17 Desemba, 2017 wameungana na waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma kusali ibada ya Jumapili.
Akizungumza baada ya Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi wote wa dini na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa kuendelea kuliombea Taifa ili lidumishe amani na upendo.
Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali anayoiongoza inatambua juhudi zinazofanywa na viongozi wa Dini katika kudumisha amani na upendo na ameahidi kuwa itaendelea kushirikiana nao katika kujenga Tanzania bora.
“Nawaomba viongozi wa madhehebu yote ya dini tuendelee kuliombea Taifa letu liwe na amani na upendo, na Serikali itashirikiana nanyi muda wote” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Padre wa kanisa hilo Fr. Sergio Madinda amemshukuru Mhe. Rais kwa ushirikiano wake na kanisa na pia amemshukuru kwa uamuzi wake wa kuhamishia Serikali Dodoma.
Katika Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 3 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kigango cha Michese na kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
17 Desemba, 2017