Licha ya Kipigo cha 4G, Yanga yaachwa na Ndege Algeria


Yanga imepata pigo lingine nchini Algeria baada ya wachezaji wake kuchelewa ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.

Wachezaji hao walikuwa wasafiri na ndege ya Uturuki kupitia Istanbul  wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa walichelewa kufika uwanjani hapo.

Wakati benchi la ufundi na wachezaji wachache wakiondoka leo, wachezaji waliochwa na ndege wanategemea kuondoka Algeria kesho au keshokutwa.

Yanga imeondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mabao 4-0 na MC Algers katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Algeria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo