Jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na jeshi la wananchi
wa Tanzania wamefanikiwa kuharibu bomu lililokuwa limetelekezwa katika
kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara vijijini baada ya
kuonekana likichezewa na watoto.
Akizungumza na vyombo vya habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Mtwara Maisha Maganga amesema taarifa hizo wamezipata kutoka kwa raia
wema baada ya kuonekana likiwa eneo la makaburi.
Amesema baada ya kupata taarifa juu ya bomu hilo
lenye kilo nne jeshi hilo lilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na
kuomba kikosi maalum cha kutegua mabomu kutoka jeshi la wananchi wa
Tanzania.
Amesema bomu hilo linaonyesha ni la siku nyingi mahali hapo na liliachwa enzi za vita ya Msumbiji.
